MKUU wa Operasheni wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Singo Benson, akizungumza na wanachama na wapenzi wa chama hicho katika
ofisi za Wilaya za chama hicho kuhusu kuahirishwa kwa maandamano na
mkutano wa chama hicho uliokuwa ufanyike jana mjini Morogoro . Picha na
Juma Mtanda
VIONGOZI, POLISI WAKUBALIANA UFANYIKE AGOSTI 8 KILOSA, FFU WAMWAGWA MITAANI KUDHIBITI WAFUASI Venance George, Morogoro BAADA
ya mvutano wa siku mbili baina ya Jeshi la Polisi na Chadema
kilichopanga kufanya mkutano mjini Morogoro jana, pande hizo mbili
zilikubaliana kuwa mkutano wa kwanza ufanyike Agosti 8, mwaka huu
Mikumi, wilayani Kilosa.Makubaliano haya yanakuja kufuatia
mazungumzo baina ya viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro na wale
wa Chadema kuwa, kwa vile maonyesho ya Nanenane mkutano huo usongezwe
mbele na ufanyike wilayani Kilosa Agosti 8, mwaka huu.
Awali
Jeshi la polisi lilizuia kwa madai kutokana na kuwapo mgomo wa walimu
nchini ambao ulisitishwa kwa amri ya mahakama Alhamisi iliyopita pamoja
na kwamba, jeshi hilo halitakuwa askari wa kutosha na kusimamia matukio
hayo.
Hata hivyo, kabla ya kufikiwa makubaliano jana hayo askari
wengi wakiwagwa mitaani kudhibiti wafuasi wa Chadema kuandamana na
kufanya mkutano wa hadhara.
Wakiwa na mabomu ya kutoa machozi,
magari yenye maji ya kuwasha, silaha za moto na virungu, vikosi hivyo
vilikabiliana na baadhi wafuasi hao kwenye mitaa mbalimbali mjini hapa
na kufanikiwa kuwatia nguvuni baadhi yao.
Hali hiyo ilitokana na
wafuasi hao kumiminika kwenye ofisi za Chadema mjini hapa kwa ajili ya
kuandaa maandamano hadi kwenye Viwanja ambavyo walitarajia kufanyia
mkutano wa hadhara.
Wafuasi hao wa Chadema pamoja na viongozi wa
ngazi mbalimbali walishiriki kwenye vuguvugu hilo ambalo chama kimelipa
jina Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), licha polisi kutoa onyo kuwa
wasithubutu kufanya maandamano na mikutano hiyo, kwa kile walichodai ni
kutokuwa na askari wa kutosha wa kutoa ulinzi.
Jana asubuhi, Jeshi
la polisi lilitawanya askari wake kwenye mitaa mbalimbali ya Mji wa
Morogoro na barabara zote za kuingia na kutoka katika mji huo.
Magari
yenye maji ya kuwasha pamoja na yale yaliyopakia askari wa FFU,
yalionekana yaranda randa katika mitaa ya Mji wa Morogoro huku
yakipeperusha bendera za rangi nyekundu kuashiria hali ya hatari.
Taarifa
zilizopatikana mjini hapa zilidai kuwa vikosi hivyo vya askari zaidi ya
200 waliletwa hapa kutoka mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam na kuungana
na wenzao wa Morogoro.
Hata hivyo, hali hiyo haikuwaogofya wafuasi
na wapenzi wa Chadema, kwani walionekana wakiendelea na maandalizi ya
kujikusanya huku wengi wao wakiwa wamevaa sare na kubeba bendera za
chama hicho.
Wafuasi hao walionekana wakiwa katika makundi kwa makundi wakielekea kwenye ofisi za wilaya za Chadema zilizoko Mtaa wa Kingo.
Hali
hiyo iliwafanya baadhi ya polisi waliokuwa katika mitaa mbalimbali
kuanza kuwakamata baadhi yao hususan pale walipoonekana kuwa katika
makundi makubwa.
Kitendo hicho kiliibua jazba na kuwafanya baadhi ya wafuasi kutoa maneno makali ya kulilaani jeshi hilo. Hali
hiyo ilionekana kuwatia zaidi hamasa wafuasi hao ambao waliendelea
kujikusanya kwa kwenye ofisi za chama huku wakihimiza kuwa waandamane na
ikiwezekana wakabiliane na yeyote atakayewazuia.
Kutokana na sakata hilo, polisi liliomba kukutana na viongozi wa Chadema wa mkoa na taifa ili kujadiliana nao.
Akizungumza
na wafuasi na wanachama walifulika katika ofisi hizo baada ya
majadiliano na polisi, Mkuu wa Operesheni za Chadema, Singo Benson
Kigaila alisema kuwa, Jeshi la Polisi limewaomba kukubali kubadilisha
ratiba na kupanga nyingine kadri chama hicho kitakavyopendekeza.
Aliongeza
makubaliano yatakwenda sambamba kuwachia huru bila masharti wafuasi
zaidi ya 10 walikuwa wamekamatwa pamoja na magari ya chama hicho.
Alisema
Jeshi la polisi limeomba maandamano na mkutano huo uliopangwa kufanyika
jana usitishwe kupisha shughuli za maonyesho ya wakulima ya Nane Nane,
Kanda ya Mashariki yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere,
mkoani hapa.
Alisema kuwa, kufuatia makubaliano hao waruhusiwa
kufanya uzinduzi M4C kuanzia Jimbo la Mikumi, wilayani Kilosa Agosti 8
mwaka huu na kuendelea katika majimbo mengine tisa yaliyosalia.
Hata
hivyo, Chadema imepanga kufanya mkutano mkubwa katika Jimbo la Morogoro
mjini ambao utawahusisha viongozi wa kitaifa na wabunge Agosti 18,
mwaka huu.
Kwa mujibu wa Chadema, maandamano hayo yatapambwa na watembea kwa miguu waliobeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Yalielezewa kuwa yatasindikizwa na misafara ya baiskeli, pikipiki, magari na helikopta ya chama hicho.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustin Shilogile alithibitisha kufikiwa
kwa makubaliano hayo na kwamba, jeshi hilo litandelea kuimarisha ulinzi
popote mikutano hiyo itakapofanyika.
|
No comments:
Post a Comment