Saturday, June 15, 2013

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM LAKUSANYA MAMILIONI YA PESA KWA MAKOSA MBALI MBALI

kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari.
                     kamishna wa polisi kanda maalum Suleiman Kova ( Picha na maktaba yetu)


JESHI LA POLISI KANDA MAALUM KUPITIA KITENGO CHA USALAMA BARA BARANI , LIMEENDELEA NA MSAKO MKALI JUU YA  MADEREVA   WANAOKIUKA  SHERIA ZA BARABARANI , NA JUML A YA YA MAGARI ELFU MBILI,MIA SABA NA THEMANINI NA SABA ,YAMEKAMATWA KWA MAKOSA MBALI MBALI .

AKIONGA NA WAANDISHIWA HABARI ,KAMISHNA WA POLISI  KANDA MAALUM SULEIMANI KOVA  AMESEMA JESHI HILO LIMEKUSANYA PESA TASLIMU ZA KITANZANIA,  MILIONI THEMNINI NA TISA, LAKI MBILI NA   ELFU THAMANINI  KUTOKANA NA TOZA  KWA MADEREVA  HAO ,NA TAYARI MADEREVA WATANO WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI .

HATA HIVYO MSAKO BADO UNAENDELEA  KWA MADEREVA WANAOVUNJA SHERIA ,NA BAADHI YA MADEREVA WALIKOMATWA WALITOZWA FAINA  PAPO HAPO,KWA NJIA YA  NOTIFICATION  NA KUPATIKANA KWA KIASI HICHO CHA PESA  .

KATI YA  MAGARI  HAYO YALIYOKAMATWA, DALADALI ZILIZOKAMATWA NI ELFU MOJA MIA TATU NA TISINI NA SITA , PIKI  PIKI  MIA NNE NA  KUMI NA SITA,  MAGARI YA WATU BINAFSI, YAKIWEMO  MAGARI  YA MIZIGO YAPATAYO SITIN NA NNE  YALIYOKAMATWA  YAKIWA YAMEPAKIA ABIRIA. 

JESHI HILO PIA  LIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WA UWIZI  WA PIKI PIKI  ,WATUHUMIWA  HAO  WALIKAMATWA KATIKA ENEO LA BUGURUNI  WAKIWA NA PIKI PIKI YA WIZI ,YENYE NAMBA ZA USAJILI T 765  BXU MALI YA  SULEIMAN ALEX MKAZI WA KARIAKOO ,
WATUHUMIWA HAO NI HUSEIN JUMA  NA AMIRI MATIBWA  AMBAO WALISHINDWA KUTOA MAELEZO JUU YA UMILIKI WA PIKI PIKI HIYO  NA POLISI INAWASHILIKILA KWA  MAHOJIANO ZAIDI.

No comments:

Post a Comment