Lulu akiwasili Mahakamani hapo.
Mahakama
Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa
msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu
anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili
7 mwaka huu.
Jaji
Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali
kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha
mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai
ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.
Baada
ya kuwasilishwa maombi hayo jana ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi
mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali
maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na
badala yake yatupwe.
Alidai
walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu
maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na
kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio
maombi mapya.
Aliwashauri
mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba
maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria
kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike
kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.
Mawakili
wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama
hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea
maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa
kupelekwa.
Aliusoma
upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali
maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka
kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina
mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.
Baada ya kusikiliza mabishano hayo ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment