Tuesday, May 29, 2012

MLIPUKO WAJERUHI KADHAA KENYA

Majeruhi wakiingizwa kwenye gari la wagonjwa kukimbizwa hospitali
Watu kadhaa wamejeruhiwa nchini Kenya katika mlipuko ambao umetokea katika jumba la maonyesho karibu na jengo la Chuo Kikuu cha Mlima Kenya pembezoni mwa eneo lenye shughuli nyingi Moi.

Mlipuko huo ambao chanzo chake hakijajulikana mpaka sasa umetokea majira ya saa saba na robo mchana na kutingisha majengo yanayozunguka eneo hilo.

Jengo hilo linalojulikana kama  Assanands lilishika moto punde mlipuko huo ulivyotokea lakini vikosi vya zimamoto vimefanikiwa kuzima moto huo ambao umeunguza sehemu ya jengo.

Imeripotiwa kuwa bado kuna watu wamekwama ndani ya jengo ambalo ndani kuna maduka ya nguo.

No comments:

Post a Comment