Tuesday, May 29, 2012

SUNRISE RADIO WAENDELEZA KIPIGO CHA MAGOLI KWA KISONGO ACADEMY

Timu ya Sunrise Radio ya jijini Arusha imeendeleza wimbi la ushindi kwa timu inazokutana nazo hii ni baada ya kuichapa bila huruma timu ya Kisongo Academy goli 8.

Magoli ya Sunrise Radio yaliwekwa kimiani na IBRAHIMU JAMALI(Team captain) aliyefunga magoli matatu,RODGER NELSON(Mhasibu)aliyefunga magoli matatu pia na MUSSA KINKAYA(Producer,DJ & Presenter)aliyefunga magoli mawili.

Akiongea kwa furaha kocha msaidizi wa Sunrise Radio BEATRICE GERALD amesema amefurahishwa na ushindi huo japokuwa kikosi chake hakikuwa na Wanandinga wake wote akiwemo golikipa HAMIS ABTWAY(Haazu) na DIONIS MOYO hivyo nafasi ya golikipa kukaa NELSON SILVESTER.

BEATRICE ameendelea kusema kuwa wachezaji wengine walikuwa majeruhi kama akina ALLY SHEMDOE(Kocha mchezaji),AMX,BARAKA SUNGA,na ALLY CHARO ambao hao wote amesema mechi ya marudiano watakuwepo uwanjani.

Kwa upande wao Kisongo Academy kupitia kwa mkuu wao wa Shule wamesema wamekubali matokeo na kukiri Sunrise Radio ni wazuri hata uwanjani na sio kama walivyowazoea redioni.

Pia mkuu huyo wa shule amesema wanajipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano ili waweze kuleta upinzani siku hiyo ya marudiano ambapo inasemekana itachezwa kwenye uwanja wa SHEIKH AMRI ABEID Arusha.


SHUHUDIA BAADHI YA MATUKIO YA MECHI HIYO
KIKOSI CHA SUNRISE RADIO
 HEKA HEKA LANGONI
 KONA LANGONI MWA SUNRISE
 ALLY SHEMDOE-KOCHA WA SUNRISE
 KABLA YA KUANZA MECHI
 DUA BAADA YA MAPUMZIKO
 KOCHA MSAIDIZI BEATRICE AKINENA NA WACHEZAJI
KINKAYA,RODGER,JOSE NA MWAKA
KINKAYA KABLA YA MECHI

No comments:

Post a Comment