Daima
panapotokea vurugu au vita wanao athirika zaidi ni akina mama na
watoto, na hii ndio hali hali ilivyokuwa hii leo mjini Morogoro ambapo
Mama na mtoto, uchungu wa mwana aujuae mzazi, hapo kila mtu aliweza
namna ya kujisalimisha na moshi wa mabomu baada ya kupigwa.

Mkuu
wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) BENSON KIGAIYA akiwa
chini ya ulinzi wa Polisi wa FFU 5 huku qwengine wakinyatia kwa
pembeni. Akiambulia makofi ya mgongo na makalio.

Boda Boda akimpa maji mtoto wa kike ili aweze kunawe kupunguza moshi
wa mabomu yaliyopigwa na askari wa FFU wakati wakitawanya wanachadema
ili wasiandamane katika kituo cha mafuta cha BP Msamvu.

Huyu naye alikuwa akitembea huku gari la FFU likiwa nyuma yake baada ya kupigwa kwa mabomu eneo hilo la Msamvu.

Mmoja wa kiongozi wa Chadema akitiwa nguvuni wakati wa maandamano
hayo yanaendelea wakati wakielekea katika uwanja wa shule ya Kiwanja
cha Ndege.

Mkuu
wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) BENSON KIGAIYA akiwa
chini ya ulinzi wa gari la polisi mara baada ya kukamatwa wakati wa
zoezi la kuwapokea viongozi wa juu wa chama hicho kushindikana katika
eneo la Msamvu kwa ajili ya maandamano kuelekea kwenye mkutano wa
hadhara wa Chadema shule ya msingi Uwanja wa Ndege mkoani Morogoro.

Hawa liingia kwa namna yake huku wakiwa na bango wakiingia kwenye
uwanja huo baada ya askari wa jeshi la polisi kufanikiwa kuvunja
maandano kwa baadhi ya makundi ya wanachadema.

Mfuasi
wa Chadema akiwa na bango wakati akiingia katika uwanja wa shule ya
msingi Kiwanja cha Ndegea kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa
M4C. SOURCE: http://jumamtanda.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment