kampuni ya mtandao wa mawasiliano Tanzania,vodacom.kwa sasa inaendeleza promosheni yake ya mji hadi mji "M-pesa Tumekufikia" ukanda wa kaskazini mjini Same mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na team ya Mambo Jambo radio inayozunguka na wana vodacom kanda ya kaskazini,mkuu wa msafara Bw.kahabi amesema promosheni ya "tumekufikia" ni endelevu na inalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu huduma ya malipo ya "mpesa" sambamba na kujishindia zawadi mbalimbali na punguzo maalum kwa simu za mkononi kutoka vodacom
Promosheni hio ilianza mji mdogo wa Hedaru na itaendelea,Same mjini,Moshi mjini,Usa riverTtengeru,Arusha mjini pamoja na Babati mjini.
No comments:
Post a Comment