Saturday, September 1, 2012

Meles Zenawi kuzikwa Jumapili



Mabalozi wa nchi mbali mbali mjini Addis Ababa, Ethiopia, pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa yaliyoko mjini humo, wamekuwa wakitoa sifa na kuonyesha heshima zao kwa Hayati Meles Zenawi, waziri mkuu wa Ethiopia, aliyefariki wiki iliyopita.

Mazishi ya Bwana Zenawi yanatarajiwa kufanyika Jumapili.
Yatakuwa mazishi ya kwanza ya kitaifa kufanyika katika nchi hiyo ya upembe mwa Afrika kwa zaidi ya miaka 80 .

Viongozi kadhaa wa Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo na kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Zenawi.

Anasifika sana kwa siasa zake za kikanda tangu alipochukua mamlaka mwaka 1991 alipofanya mapinduzi dhidi ya dikteta
Mengistu Hailemariam.

Baadhi ya viongozi watakaohudhuria mazishi hayo ni pamoja na rais wa nchi jirani ya Djibouti, Ismail Omar Guelleh,
Mwai Kibaki wa Kenya na Salva Kiir wa Sudan Kusini pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Uganda
Yoweri Museveni.
Serikali za China, Marekani pamoja na Muungano wa Ulaya zinatarajiwa kutuma waakilishi wao.

No comments:

Post a Comment