
1.UTANGULIZI
Ndugu wanahabari,BAVICHA jimbo la Segerea limewaita hapa leo
06/09/2012,ili kutoa masikitiko,kulaani na kutoa tamko juu ya vitendo
vinavyoendelea kushamiri vya mauaji dhidi ya raia wasio kuwa na
hatia.vifo hivi vyenye mashaka vinavyoendelea kutokea mbele ya uwepo wa
jeshi la polisi vimeendelea kwa muda mrefu sasa bila ya kupatiwa
ufumbuzi wa kudumu,na vinazidi kuondoa imani ya jeshi hili lenye dhamana
ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
Matukio ya mauaji ya hivi karibuni yaliyotokea mbele ya jeshi la
polisi,mkoani Morogoro (Morogoro mjini) Nyamongo mkoani Mara na tukio la
kuuwawa kwa mwandishi wa habari kijiji cha Nyololo mkoani Iringa ni
baadhi tu ya matukio mengi yenye mashaka na yanayoleta sintofahamu juu
ya utendaji kazi wa jeshi la polisi na kusababisha kutokuaminika tena
kwa watanzania.
BAVICHA jimbo la Segerea tunasikitishwa sana na mauaji ya KINYAMA ya
mwandishi wa habari,marehemu DAVID MWANGOSI yaliyotokea
02/09/2012,akitekeleza majukumu yake ya kutafuta habari kwenye tukio la
uzinduzi wa tawi la CHADEMA kijiji cha Nyololo,huku akiwa amezungukwa na
polisi wengi na wasiweze kumuokoa na kifo hicho.Je kazi yao ilikuwa
nini kama siyo kulinda usalama wa raia na kama ni kulinda ilikuwaje
DAVID alikufa amemkumbatia moja ya wanausalama hawa?huku wengine
wakimshambulia?
Tunashangazwa sana na jeshi la polisi kuzuia mikutano ya ndani
iliyokuwa ikifanywa na CHADEMA kwa kisingizio cha kupisha zoezi la sensa
ya watu na makazi,wakati likiacha mikutano ya ndani ya CCM wakiendelea
na chaguzi za viongozi wa UWT na UVCCM na mikutano ya hadhara wakati
zoezi la sensa likiendelea,kwa mfano Uzinduzi wa kampeni za uchaguzi
mdogo wa mbunge jimbo la BUBUBU UNGUJA( Uzinduzi huo ulifanywa na Dr
Mohamed Ghalib Bilal,UVCCM wilaya ya Temeke na Kinondoni,UWT wilaya ya
Temeke-Uchaguzi uliofanyikia PTA hall sabasaba,Mkutano wa hadhara wa
kuwashukuru wananchi uliofanyika jimbo la Mchinga(Mh.Said Mtanda
alihutubia),Asha Suleiman Idd(mjumbe wa
kamati ya siasa wilaya ya Kaskazini B) aliekuwa akifungua mkutano wa
UVCCM katika wilaya ya Kindunina mbunge wa Bumbuli mh.January Makamba
aliefungua mkutano wa jumuia ya wazazi CCM wilaya ya Lushoto.
Wakati matukio haya yote yakifanywa na CCM ni kipindi cha muda wa nyongeza wa sensa ulikuwa ukiendelea.
BAVICHA jimbo la Segerea tunahoji,KATAZO LA POLISI LA KUZUIA MIKUTANO
NA SHUGHULI ZOTE ZA SIASA NI KWA CHADEMA TU?
Hali hii inatoa picha
kwamba jeshi la polisi linatumika kisiasa kwa kuibeba CCM,ni kwa namna
gani wataepuka kuitwa POLISISIEMU?
hata hivyo kuna dalili tosha kwamba
vyombo vya habari navyo vimeanza kujengewa hofu katika kutekeleza
majukumu yao,kwa hili la kuuwawa kwa mwandishi akiwa amezungukwa na
polisi akitafuta habari kwenye tukio la kisiasa za chadema,tunajiuliza
ni kwa vipi walishindwa kulinda usalama wake ili hali wakijua ni
mwandishi?
ni nani hasa alimuua DAVID MWANGOSI? mbele ya wanausalama
waliokuwa na silaha,magari, intelijensia,radio call,kofia za
kujikinga,marungu,mabuti na vyote walivyotakiwa kuwa navyo? Mauaji haya
ya KINYAMA katikati ya polisi wengi yanatudhihirishia kwamba wizara hii
ya mambo ya ndani inayoongozwa na Emmanuel Nchimbi pamoja na mkuu wa
polisi IGP MWEMA wameshindwa kabisa kukomesha tabia ya vifo vya raia
vyenye utata na hasa pale vinapotokea mikononi mwa polisi,na kwamba wao
ni wadau halali wa kifo cha marehemu DAUD MWANGOSI. BAVICHA SEGEREA
TUNATAMKA KWAMBA
1.TUNAMTAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI AJIHUZULU KWA
KUSHINDWA KUZUIA VIFO VYA RAIA WASIO NA HATIA VINAVYOTOKEA MIKONONI MWA
JESHI LA POLISI ,HASA KWA MAUAJI YA MWANDISHI YALIYOTOKEA AKIWA
AMEZUNGUKWA NA POLISI WENGI TU.
2.TUNAMTAKA RAIS JK AVUNJE UKIMYA SASA JUU YA TABIA HII YA MAUAJI YA
RAIA WASIO NA HATIA KUUWAWA MBELE YA POLISI, KWA KUWAFUKUZA KAZI MARA
MOJA IGP SAID MWEMA,MKUU WA OPERATION PAUL CHAGONJA NA RPC WA IRINGA
KAMUHANDA ,NAHATA HIVYO RAIS NI MWEPESI SANA KUTOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI
KWA MISIBA INAYOGUSA TAIFA, NI VIPI KWA KIFO CHA DAUD BADO YUKO KIMYA?
3.POLISI KAMA WANAJIFUNZA KUUA RAIA WASIO NA HATIA BASI NASISI
TUTAHAMASISHANA KUJIFUNZA KUFA,NA HATUTAOGOPA TENA KUFA KWA KUWA
TUNAJUA TUSIPOKUFA LEO,TUTAKUFA KESHO NA TUSIPOKUFA KESHO IPO SIKU
TUTAKUFA.
4.SERIKALI YA CCM IACHE KUTUMIA NGUVU YA DOLA KUTISHA ,KULETA HOFU
WALA KUDHOOFISHA WANANCHI WASIENDELEE KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA
CHADEMA,NA TUNA MTAKA KATIBU WA UVCCM TAIFA,MARTIN SHIGELA AACHANE NA
PROPAGANDA ZENYE LENGO LA KUPOTOSHA UMMA NA KUTISHA VIJANA WASIKIUNGE
MKONO CHADEMA.
5.BAVICHA SEGEREA TUNATANGAZA KUTOKUWA NA IMANI NA MSAJILI WA VYAMA VYA
SIASA,NA TUNAMTAKA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JOHN TENDWA AUELEZE UMMA
KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KAULI YAKE,NA KAULI YA WASIRA NA KAULI YA
WAZIRI MKUU BUNGENI(AMBAYO NI YA SERIKALI NA NI YA CCM PIA) ILIYOLENGA
KUTISHIA KUIFUTA CHADEMA,ILI HALI WAKIJUA WANAOUA WATU SIO CHADEMA BALI
NI JESHI LA POLISI? NA ATUELEZE JE TENDWA NAE ANAKOSA AMANI KUFUATIA
CHADEMA KUUNGWA MKONO NA WANANCHI HUKO VIJIJINI? NA MAENEO MENGINE
NCHINI.
6.BAVICHA JIMBO LA SEGEREA TUNATOA RAI KWA VIJANA WOTE TANZANIA
WANAOHITAJI MABADILIKO NA WENYE MTIZAMO CHANYA WA UKOMBOZI KUTOKA
MIKONONI MWA MAFISADI, KUWA TAYARI KUPAMBANA NA NAMNA YOYOTE YA
UONEVU,UKANDAMIZAJI,UDHALILISH AJI NA UBAGUZI WA NAMNA YOYOTE ILE.
No comments:
Post a Comment