
Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba
--
‘‘Mauaji Ya Waandishi Na Wananchi YatavurugaMchakato Wa KupataKatiba
Mpya Tanzania!’’
JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumepokea taarifa za kuuawa kinyama
kwa Mwandishi Daudi Mwangosi wa Channel 10 na Mwenyekiti wa Chama cha
waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) kwa mshtuko na masikitiko
makubwa. Kama ilivyokwishaelezwa na wengi, kifo cha mwandishi huyu ni
cha kwanza cha aina yake katika tasnia ya habari nchini na kinatishia
si tu uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa habari kwa ujumla wake, bali pia
kifo hiki na vingine vya siku za karibuni vinauweka mchakato wa Katiba
Mpya njia panda.
Vitendo vya mauaji ya raia vinazidi kushamiri siku hadi siku. Wapo
wananchi wanaouawa na watu wanaoitwa wenye hasira kali kwa tuhumaza
uhalifu. Wapo raia wanaouliwa na majambazi na wahalifu wenginekwa sababu
ya ulinzi duni katika maeneowanayoishi.
Aidha, wapo pia wananchi wanaopoteza maisha yao kila siku kwa tuhuma za
kwamba ni wachawi.Ukiacha hao, idadi kubwa ya watanzania wanaishi na
ulemavu wa ngozi wamepotezamaisha kwa kukatwa viungo au kuuliwa kabisa
kwa imani za kishirikina.
Hali sasa imefikia kuwa mbaya hadi kuna watanzania wanajisikia salama
zaidi wakiwa mwituni kuliko majumbani. Yote haya yanasikitisha sanakwa
ujumla wake! Haki ya kuishi
inayowekwa na kulindwa na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania imeanzakuingia dosari katika Tanzania.Ukiacha mauaji
yanayofanywa na watu wasiojulikana au miongoni mwa raia, yamekuwepo pia
mauaji yanayozidi kuongezeka ya raia yanayofanywa na wawekezaji au
matajiri nchini. Zipo kesi kadhaa za mauaji ya namna hii.
Hayo nayo yamekuwa yakitokea kwa sababu ya ulinzi mdogo ambao wananchi
wanao kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Jeshi la Polisi,
ambalo ndio lenye dhamana ya kulinda watu na mali zaohaliwezi kukwepa
lawama katika aina zote hizo za mauaji. Itakumbukwa pia kuwa ajali za
magari, mabasi na meli zinagharimu sanamaisha ya watanzania katika siku
za karibuni.
Kwa kiasi fulani, hata kukithiri kwa ajali hizi nako kunahusishwa na
mwenendo mbovu wa usimamizi wa vyombo vya usafiri unaofanywa na idara
mbalimbali za serikali ikiwemo kikosi cha usalama barabarani. Roho
zawatanzania zinazidi kupotea kutokana na udhaifu
mkubwa unaosababishwa na rushwa na mambo mengine ya ukosefu wa maadili
katika vyombo vya usimamizi wa haki. Mauaji ya raia yanayofanywa moja
kwa moja na askari wa Jeshi la Polisi nayo yanazidi kuongezeka sanakiasi cha kutishia amani na utulivu wa nchi yetu.
Aidha, mauaji yanayohusishwa na siasa nayo yanazidi kuongezeka na kuzidisha chuki ya
kisiasa ambayo ni mbaya sana kwa ustawi wa nchi yetu. Kwa mfano katika
miezi ya Karibuni, kumekuwepo matumizi ya nguvu kuzidi kiasi kwa raia
wanaokuwa wakipanga na kufanyamaandamano au mikusanyiko yenye lengo la
kujadili au kupinga jambo fulani. Matokeo yake, kumetokea majeruhi na
mauaji ambayo yamesababishwa na vurugu ambazo zinatokana na Jeshi la
Polisi kudhibiti vitendo halali vya wananchi.
Kwasababu hiyo, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunatoa witoufuatao kwa Jeshi
la Polisi na idara nyingine za serikali zenye dhamana ya kulinda usalama
wa raia, malina
mipaka ya Nchi yetu:
1.1. Jeshila Polisi liache kutumia nguvu kuzidi kiasi katika matukio
yote ya kulinda mikutano na matukio ya hadhara. Tujuavyo sisi, Jeshi la
Polisi linalotumia risasi za moto, mabomu ya kivita, maji ya kuwasha na
gesi ya kutoa machozi dhidi ya raia ambao hawajabeba hata
fimbo za kuchungia mifugo.
Ni Jeshi lisilojiamini na linaloonesha woga wa ajabu. Kwa hadhira kama
za Nyololo, Morogoro, Mbeya, Dar es Salaam na nyinginezo miezi
ya Karibuni, Jeshi la Polisi lingeweza kuwatuliza
wananchi kwa kutumia filimbi tu. Matumizi ya nguvu na kumwagia maji ya
kuwasha hata wazee wastaafu wanaodai haki zao inaweza kuwa ndio laana
inayopelekea Polisi kusikia furaha kuua kila mara.
Ipo kanuni ya kimataifa inayowataka Polisi kutumia nguvu kidogo sana inayolingana tu
na nguvu ya umma wanaokabiliana nao katika kutuliza ghasia.
2.Wakati huu wa mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania na hata
baada ya hapo, Jeshi la Polisi lijiepushe kuingilia shughuli za Kisiasa
kwa kuziunga mkono au kuzivuruga. Mikusanyiko mingi ambayo imepelekea
mauaji wakati polisi ikijaribu kuivunja ni matukio yaliyolenga kupata
majibu ya kisiasa na siyo ya kipolisi. Wajibu wa
Jeshi la Polisi
katika wakati kama huo ni kulinda na kuwezesha wananchi husika kueleza
madai yao kwa uhuru na bila kuvurugwa na kundi jingine lolote la watu
wasiopendezwa na madai ya kundi husika. Tabia inayozidi kushamiri ya
Jeshi la Polisi kutaka kujibu au kuzima hoja za Kisiasa au kiuchumi kwa
mtutu wa bunduki, mabomu, maji ya kuwasha na virungu ni tabia ya
Jeshi kutaka kuingilia kazi isiyo yake na ndio maana inawashinda. Aidha,
kama Polisi wangekuwa niwataalam wa Siasa, wangegundua kuwa
wanachokifanya ni kuahirisha matatizo na si kuyatatua!
3. Jeshi la Polisi na vyombo venye dhamana ya ulinzi vijitambue upya
kuwa vina wajibu wa kulinda raia, mipaka na mali zao si vinginevyo.
Mauaji yanayoendelea nchini ni uporaji wa haki ya kuishi na haki
nyingine nyingi chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana ile
ya Zanzibar.Aidha, Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla wana
wajibu wa kuhakikisha na kudumisha ustawi wa wananchi kwa mujibu wa ibara ya 8 (1) (b) nahawana mamlaka ya kuua raia.
Ikumbukwe kuwa mamlaka yote kikatiba katika Tanzaniayako kwa wananchi na serikali
pamoja na Jeshi lake la Polisi watapata madaraka na mamlaka hayo kutoka
kwa Wananchi. Nani amewapa Polisi mamlaka ya kuua watanzania? Nani
amewapa Jeshi la magereza mamlaka ya kuwapiga na kumwaga damu za
Waandishi? Nani amewapa askari wanyamapori mamlaka ya kupiga risasi
hovyo nakuua ng’ombe mbele ya wenye maliyao?
4.Athari za matukio ya mauaji na fujo zinazosababishwa na Jeshi la
Polisi kutawanya waandamanaji au mikusanyiko mingine ni kubwa sana
katika kuathiri vibaya hamasa ya wananchi kwenye Mchakato wa Katiba.
Mpaka sasa, tayari watu wengi wameingia wasiwasi na wameamua kutoshiriki
mikutano ya kutoa maoni ya Katiba inayoendeshwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba nchini.
Endapo Jeshi la Polisi halitaacha kuua na kutishiaraia kwa kila
wanachokifanya, mchakato wa Katiba utavurugika kabla Katiba mpya
haijapatikana. Kwa mwenendo wa sasa, Jeshi la Polisi litakuja kupiga
mabomu na kuua hata wananchi watakapokuwa katika Mabaraza ya Katiba
wakijadili na kupinga baadhi ya vipengele vitakavyoingizwa katika rasimu
ya Katiba. Pia, itafika wakati wananchi watataka kuandamana kwa amani
kuunga mkono au kupinga mambo Fulani katikaKatiba. Kwa hali ilivyo,
Jeshi la Polisi litaona hiyo ni fursa
ya kutumia mabomu na risasi kuzuia wasiseme wanayotaka kusema. Hii ni hatari kubwa sana!
5. Mikusanyiko, maandamano na shughuli za mikutano ya Siasa ni matendo
halali na haki ya kila mtanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano, 1977 ibara ya 8, 20 na 21. Suala la kutoa taarifa kwaJeshi la
Polisi kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Polisi ni suala la
kuwajulisha tu kwa lengo la kuwaweka tayari endapo kutahitajika msaada wa Jeshi la Polisi wakati wa shughuli kamahiyo.
Tabia iliyoota mizizi ya Polisi kujiona kama wamepewa taarifaili watoe au kukataa kibali ni
uelewa finyu wa Katiba na sheria za Nchi. Ipo haja ya kuongeza uelewa wa
wasimamizi wetu wa sheria ili wawe na uelewa mpana wa sheria na ibaraza
Katiba wanazozisimamia badala ya kujiona kama wana wajibu wa Msajili wa
vyama vya Siasa wa kuratibu shughuli za vyama. Mikutano, mikusanyiko,
mihadhara, maandamano na mijadala ni haki ya Kikatiba ya
Kila mtanzania binafsi na kwa makundi.
Kwa kuwa haki ya kuishi iliyoporwa kwa MwandishiDaudi Mwangosi ndio haki
kubwa kuliko zote, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunataka jambo hili
lisiishiekuunda Tume za
uchunguzi pasipo kufanyia kazi mapendekezo yake. Aidha, kwa kuwa
uchunguzi unaofanywa hauhusiani na kilichomuua ndugu Mwangosi wala kundi
gani limemuua, tunapendekeza busara itumike kwa viongozi wa Jeshi la
Polisi, kuanzia Kamanda wa Polisi Mkoawa Iringa kuachia ngazi ili
kupisha uchunguzi huru wa Tume itakayoundwa na Mheshimiwa Rais
ikihusisha na kuongozwa na mhimili wa Mahakama. Taarifa ya uchunguzi
ipelekwe Bungeni na Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kujadiliwa na ushauri
wa kibunge.
Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tunaitamka rasmi
kuwa batili kwa kutumia kanuni ya sheria za kiasili inayosema kuwa mtu
au kundi hawezi kuwahakimu wa kesi inayomhusu mwenyewe. Bila kufanya
hivyo, tunapata wasiwasi kama Tume ya namna
hiyoinaweza kufanya kazi yake kwa uhuru. Kuachia ngazi kwa Kamanda wa
Polisi mkoani Iringa kutakuwa ishara kuwa Jeshi la Polisi linahitaji
kuwa makini zaidi katika kufanya kazi yake ya kulinda amani, mali na
maisha ya watanzania. Kwa sasa, zipo hisia kuwa Jeshi la Polisi lipo juu
ya sheria na Katiba, jamboambalo tunapenda kulikanusha vikali!
Mwisho, tunapenda kutoa rai kwa serikalikutangaza rasmi kuwa itachukua
jukumu la kutunza, kusomesha, kulisha na kuhudumia familia aliyoiacha
Daudi Mwangosi kuanzia sasa kwa muda wa miaka 20 watakapoweza
kujitegemea wenyewe. Itakuwa ni fedheha kuiona familia aliyoianzisha
Marehemu Mwangosi ikisambaratika kwa sababu kichwa cha nyumba hiyo
kimesambaratishwa na bomu la Polisi ambalo kodi yake Mwangosiilichangia
kulinunua. Kufikia hapa, tunapenda kutangaza rasmi kuwa msiba huu
nimsiba wa KIKATIBA na tunaomba ufahamike hivyo kwa umma wote wa
watanzania na kote duniani.
Mungu ailazeroho ya Marehemu Mwanahabari Daudi Mwangosi mahali pema
peponi Amina!
Imetolewana kusainiwa kwa niaba ya JUKWAA LA KATIBA TANZANIA,
Deus Kibamba
Mwenyekiti
Alhamis, 06 Septemba 2012
No comments:
Post a Comment