Matamshi hayo ya Iran yaliotolewa leo na msemaji wa Wizara ya mambo ya nchi za nje Ramin Mehmanparast, yanaonyesha kuendelea kusisitiza kwa Iran kwamba inaweza kukabiliana na shinikizo la nchi za magharibi lenye lengo la kuzuwia hatua ya Iran ya urutubishaji wa madini ya uranium.
Umoja wa Ulaya wenye nchi 27 wanachama jana ulitangaza hatua mpya ya vikwazo dhidi ya Iran ukipiga marufuku uagizaji wa gesi ya Iran na kuweka vikwazo vyengine vya biashara na shughuli za fedha.
Nchi za magharibi zinahofia kwamba Iran ina lengo la kutengeneza silaha za nyuklia, lakini Iran inasema mradi wake ni kwa ajili ya matumizi ya amani na hasa nishati.
No comments:
Post a Comment