Umoja wa Ulaya watakiwa kuzingatia wakimbizi kutoka Syria
Umoja wa Ulaya unapaswa kuandaa mpango kwa ajili ya idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Syria, hata kama mmiminiko wa wahamiaji umekuwa ni mdogo.
Shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR, pia limeukosoa Umoja wa Ulaya kwa kutekeleza sheria za ukimbizi kwa njia isiyofanana.
Kwa mfano nchini Ugiriki, utaratibu unaotumika kwa wanaoomba ukimbizi umeshindwa kulinda mahitaji ya wakimbizi wengi.
Msemaji wa Shirika hilo la Umoja wa mataifa Adrian Edwards amesema baadhi ya nchi za mashariki wanachama wa Umoja wa Ulaya zinawakataa zaidi ya 50 asili mia ya wakimbizi kutoka Syria .
No comments:
Post a Comment