Kiongozi wa waserbia wakati wa vita vya Bosnia Radovan Karadzic, ameanza kujitetea leo katika kesi inayohusu mashitaka 10 yanayomkabili mbele ya mahakama ya kimataifa mjini The Hague.
Mashitaka hayo ni pamoja na mauaji,uhalifu wa kivita na maovu dhidi ya binaadamu,Karazdic aliye na umri wa miaka 67 anashutumiwa kwa kuhusika na mauaji mabaya kabisa katika historia ya Ulaya baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.
katika kampeni ya kuwamaliza waislamu na wakroatia wa Bosnia, Kiasi ya watu 100,000 waliuawa katika vita vya 1992-1995 na wengine milioni 2.2 wakalazimika kuyahama makaazi yao.
No comments:
Post a Comment