Wednesday, October 17, 2012

Marekani ingali inazalisha kwa wingi silaha za nyuklia


Marekani ingali inazalisha kwa wingi silaha za nyuklia
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Nyuklia kwenye maabara ya taifa huko New Mexico nchini Marekani amesema kuwa, matamshi ya viongozi wa Marekani ya kutaka ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia ni uchochezi na uongo wa wazi.
Jay Coghlan amesema kuwa, wananchi wa Marekani hadi sasa hawaelewi kwamba Washington inaendeleza biashara ya silaha za nyuklia. Ameongeza kuwa, maabara ya Los Alamos National Laboratory ni moja kati ya maabara kuu za kielimu katika masuala ya silaha za nyuklia katika jimbo la New Mexico, nchini Marekani.  

 Jay Coghlan  ameongeza kuwa, kinyume na nara na kaulimbiu zinazotolewa na Marekani na nchi nyingine za magharibi juu ya kuwepo ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia, hivi sasa Marekani inatengeneza na kuzalisha silaha za nyuklia kwa uficho zikiwa katika sampuli mbalimbali.


Inafaa kuashiria hapa kuwa, miaka minne iliyopita, Rais Barack Obama wa Marekani akiwa mjini Prague, Jamhuri ya Czeck alisema kuwa, Marekani  inazo silaha za nyuklia, lakini inapiga hatua kuelekea kwenye ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia.

No comments:

Post a Comment