Maafisa wa Libya wanasema kuwa mewatia nguvuni wafungwa 60 kati ya mia moja na ishirini na wawili waliokuwa wametoroka jela katika mji mkuu Tripoli .
Maafisa sasa wanadhibiti magereza kadhaa , likiwemo gereza la Al-Jadaida lililo maalum kwa wahalifu wa kawaida .
Zaidi ya wafungwa 100 walitoroka kutoka jela la Al-Judaida mjini Tripoli.
Wafungwa hao wanasemekana kuwa raia wa nchi mbali mbali na maafisa wanasema kuwa takriban watu 60 wamekamatwa.
Haijulikani ni vipi wafungwa hao walifanikiwa kutoroka jela.
Al-Judaida ni mojawapo ya jela kubwa zaidi mjini Tripoli. Mashirika ya kutetea haki za binadamu wanatuhumu maafisa wa magereza kwa kuwatesa wafungwa.
Tukio hilo la wafungwa kutoroka, linajiri chini ya wiki moja kabla ya kuadhimishwa mwaka mmoja tangu kuuawa kwa kanali Gaddafi.
Kiongozi wa jeshi la Libya, Khaled al-Sharif, aliambia BBC kuwa kati ya wafungwa 120 ambao walitoroka , nusu yao wamekamatwa.
Aliongeza kuwa baadhi ya wafungwa hao walikuwa wahamiaji haramu wa kiafrika, na wengine walikuwa raia wa Libya waliofungwa kwa makosa ya uhalifu.
Hali inayozingira tukio hilo ni tete kwa sasa na maafisa wanasema kuwa uchunguzi unafanywa kwa sasa.
Idara ya ulinzi wa ndani imeweka vizuizi barabarani katika eneo hilo kujaribu kuwasaka wale waliotoroka.
Ulinzi umedhibitiwa katika magereza hayo.
No comments:
Post a Comment