Wednesday, October 31, 2012

wimbo mpya wa diamond utata mtupu


Wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya Hamis Ramadhan aka H.Baba pamoja na Pasha wamemlalamikia msanii mwenzao Naseeb Abdul 'Diamond Plantnum' kutumia idea yao pamoja na jina la nyimbo 'Nataka Kulewa'

Malalamiko hayo yameibuka hivi karibuni baada ya Diamond kuachia wimbo huo na kusababisha utata mkubwa kwa wasanii wawili hao tofauti huku Pasha akidai kuwa msanii huyo 'Diamond' katumia beats ya nyimbo yake aliyomshirikisha Tunda Man  'Amekuwa'

Huku kwa upande wake H. Baba amedai msanii huyo kutumia idea ya nyimbo pamoja na jina la wimbo huo,

Akizungumza na mwandishi wa habari hii H. Baba alisema kuwa ameshangazwa na kitendo cha msanii huyo kutumia jina la wimbo wa kwake 'Nataka kulewa' huku kiitikio cha nyimbo hiyo kuwa na mfanano sawa wa nyimbo yake

"Wakati mimi nipo studio na KGT nikirekodi wimbo niliomshirikisha Q Chief ndipo Diamond alifika hapo studio na aliisikia kiitikio cha wimbo wangu pamoja na jina la wimbo wangu na aliusifia ila cha kushangaza yeye tena katumia jina la wimbo wangu pamoja na idea yote" alidai H. Baba

H. Baba alipoulizwa kuhusu hatua gani ameichukua baba ya kudai kuibiwa nyimbo na Diamond alisema kuwa yeye ameamua kuwaeleza jamii ukweli kuhusu nyimbo hiyo na anasubili msanii huyo kumfuata kwa ajili ya kujieleza kwake

Alisema kuwa hayuko teyari kugombana na msanii huyo kwa madai kuwa Diamond ni mchanga kwenye gemu ya muziki kwa kuwa anamiaka mitatu tofauti na yeye mwenye miaka 9 kwenye upande huo wa sanaa huku akiwa anatunga nyimbo zake mwenyewe

Msanii huyo alisikitika kwa kueleza kuwa hajui wasanii wanaelekea wapi kwani kuiba kazi ya msanii mwenzio siyo kujijenga kiusanii bali ni kujibomoa

Kwa upande wake Pasha ambaye na yeye inasemekana kuwa Diamond ametumia beat ya nyimbo yake alisema kuwa ameshangazwa na kitendo alichofanya msanii huyo na alikuwa na madhumuni gani

"Ukisikiliza nyimbo yangu kwenye upande wa beat na melodi kiujumla na ukisikiliza nyimbo ya Diamond hauwezi kuutofautisha sasa sijui tunaelekea wapi" alisema Pasha

Pasha alipoulizwa kuhusu hatua alizochukua alisema kuwa alichukua hatua za awali za kumpigia simu Diamond pamoja na Mtayarishaji wa muziki wa msanii huyo lakini hatua hiyo haikuweza kuzaa matunga kwa sababu hawakupokea simu

Mwandishi wa habari hii alimpigia simu Diamond ili kudhibitisha madai hayo ila haikuzaa matunda mazuri kwani simu hiyo haikupokelewa na baadaye kuzimwa kabisa

Malalamiko hayo yametokea baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond plantnum kuachia ngoma mpya ya 'Nataka Kulewa'


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

No comments:

Post a Comment