Wednesday, November 7, 2012

Mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea Nigeria



Mafuriko Nigeria
Zaidi ya watu milioni mbili nchini Nigeria waliathirika kutokana na mafuriko na hivyo kulazimika kutoroka makwao mwaka huu
Idara ya kukabiliana na majanga nchini humo,(Nema) inasema kuwa mvua kubwa zilisababisha vifo vya watu 363 tangu mwezi Julai.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria, Will Ross anasema kuwa maji yameanza kupungua lakini bado kuna hofu ya kupungua kwa chakula kwani wakulima waliharibikiwa na mazao yao mashambani.Hayo ndiyo yalikuwa mafuriko mabaya zaidi katika miaka hamsini kuwahi kutokea nchini humo na yameathiri maeneo mengi ya nchi hasa maeneo yaliyo katika mto Niger.
Rais Goodluck Jonathan mwezi jana, alitaja mafuriko hayo kama janga la kitaifa lakini alisema kuwa tatizo hilo halitasababisha ukosefu wa chakula.
Duru zinasema kuwa ukosefu wa nyenzo za kuzuia mafuriko ndio tatizo kubwa katika miji mingi ambayo imeshuhudia mafuriko baada ya mvua kubwa.
Katika maeneo mengine ya mashinani watu walielezea hofu ya kuingiliwa na wanyama kama mamba, nyoka na hata viboko ndani ya nyumba zao.

habari kaw hisani ya BBC SWAHILI 

No comments:

Post a Comment