Friday, April 26, 2013

MADEREVA NA MAKONDAKTA JIJINI ARUSHA WAIOMBA SERIKALI KURUDISHA BEI YA NAULI KUWA SH. 300/= KAMA MWANZO KWANI WANAPATA HASARA BAADA YA ABIRIA KUAMUA KUWA HAWAPANDI DALADALA BADALA YAKE WANATEMBEA.







Kuanzia kushoto ni Mr Adam toka Canada ambaye ni mwandishi wa habari aliyeegemea sana kwenye habari za Mambo ya haki za binadam ambaye tuko naye MJ radio kwa miezi kadhaa kubadilishana ujuzi, Jumalee Mngano, Kikoricho, Bilhuda Msangi, Deo Limo na Jamaal Masoud kabla ya kuingia mtaani


safari huanza na mipango




haazu akimuhoji dereva wa daladala
Kama Kawaida kwa May C ni kama mtaa wa pili vile akawa Karibu na kina mama wanaofanya biashara ndogondogo stand Ndogo ya vidaladala nao wakafunguka adha wanayoipata kwa gharama ya maisha kupanda kila kukicha






Kushoto ni MR. Adam Kutoka Canada














Hatukuwaacha wapiga debe nao walifunguka kuwa hakuna abiria


Kutoka kushoto ni haazu, jumalee Mngano, May C, Mr adam toka Canada na Kikoricho


Kikoricho akiongea na konda wa daladala




Jamaal Masoud akiongea na Abiria
May C akimuhoji Selemani ambaye anafanya biashara ndogo ndogo eneo la kilombero Arusha
Jumalee Mngano akimuhoji Jamaa maarufu kama Mpiga Debe a.k.a Msaka Jala kutaka kujua mawili matatu toka kwao


HABARI NA HAMIS ABTWAY (HAAZU MJ RADIO ARUSHA)



Mapema Leo Wafanyakazi wa MAMBO JAMBO RADIO (MJ RADIO 93.0 FM) Tumeamua kuingia mtaani kuongea na Wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili Wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na hali ya ugumu wa maisha pamoja na kuangazia Suala zima la Kupandishwa kwa nauli na gharama za Usafirishaji.





Katika Harakati za kutaka kujua haswa wananchi, Madereva na Makondakta kuna nini kinachofanya kila mmoja wao ananung’unika na kufikia hadi hatua ya kuwepo kwa matukio na visa vidogo vidogo vya kati ya makonda na Abiria kufuatia kupandishwa kwa Nauli kitu ambacho kinawafanya abiria kugombana na Makonda ambapo huko Kwa pamoja tumekuja kugundua kuwa kuna mengi ambayo yanaendelea kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mikwaruzano mikubwa kati yao ambapo mara nyingine suluhu inakuwa ni Vituo vya Polisi.





Ni hivi majuzi tu ambapo SUMATRA wamepandisha nauli za Daladala kutoka sh. 300/= hadi sh. 400/= kwa kituo kimoja hadi kingine kitu ambacho kinawafanya wananchi kuilalamikia Serikali kwa kusema kuwa haiwajali.





huyu ni mzee wa miaka 72 ambaye naye anaiomba serikali kuangalia upya suala la gharama za maisha na hali ya mwananchi wa kima cha chini
Wanahabari wa MJ tumepata kuongea na Abiria, Madereva na Makondakta ambapo Wote kwa pamoja wamesema kuwa hawaoni haja ya kuongezwa kwa nauli.





WANANCHI


Katika wananchi ambao tumepata kuongea nao wengi waliisukumia Serikali lawama kuwa serikali yao ndiyo haiwajali kwani Inajua ni jinsi gani hali ya uchumi wa Tanzania kwa Mwananchi wa Chini ulivyo kwa sasa.





MAMA MERY, SELEMANI, VINCENT, DK KAZIMOTO  NA JOHNni baadhi ya Wananchi ambao tumeongea na wao kuitupia Serikali lawama hizo ambapo kama MAMA MERY yeye ni mama anayefanya kazi ndogo ndogo ya kuuza mchicha na anapata Sh. 3000/= kwa siku akilipa nauli yake mwenyewe kwenda na kurudi anapofanyia biashara yake  anatumia sh. 800/= ana watoto watatu wanafunzi ambao wanatakiwa wale, wavae, wanywe na Awape nauli y ash. 1000 kwa wote kwa siku…..hapo hajachakaza mwanafunzi sare ya shule, daftari wala kalamu haijaisha kitu ambacho kiukweli unaweza ukamuhurumia.


Kila mmoja ameongea mengi ila kikubwa hawajapendezwa na kitendo cha kupandishwa kwa nauli bila sababu kwani wanajua kuwa mafuta hayajapanda hivyo wanaamini sio sahihi na hawatendewi haki.
Huyo hapo ni Dk. Kasimoto Kutoka Monduli anyeuza dawa za asili Jijini Arusha


Jamaal Masoud akiongea na mama Mary (abiria)


USHAURI WAO


Tumepata kuwauliza mfano wangepata nafasi ya kukutana na uongozi wa juu akiwemo Mh. Rais JK Kikwete kwamba wangemuomba nini na  wao wakasema Kuwa wanaomba Rais aangalie hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida na kuwa wakati pia inapangwa mipango yoyote ni vyema pia wangeangali Mwananchi wa Kawaida ana faidika au anaumizwa na pia sio mbaya wakijribu kupata Maoni toka kwa Mwananchi wa kawaida kuliko kupandisha vitu wakati wanajua wazi kuwa hli ya kiuchumi ni ngumu.





MADEREVA NA MAKONDAKTA WASEMA HAWAONI SABABU YA NAULI KUPANDISHWA.

Konda wa daladala akitoa ushirikiano





Katika mazungumzo yetu na Madereva na Makondakta wengi tuloongea nao wamesema hawaoni sababu ya Nauli kupandishwa kwani wao wenyewe hawafaidiki chochote zaidi ya hasara wanayopata kwa sasa kila kukicha.





ABIRIA HAWAPANDI TENA MAGARI WANATEMBEA KWA MGUU…..HASARA KWA MAKONDA NA MADEREVA





Madereva na Makonda wanalalamika kuwa kwa sasa hawapati chochote kwani hakuna abria wengi tena kwa kuwa abiria wengi wameona kuliko kulipa sh. 400 kwa kituo kimoja bora kutembea hivyo kufanya wao kama Madereva na makonda kukosa abiria Wakati ambapo Mabosi wao wanataka jioni ukabidhi hesabu kama inavyotakiwa.





WAMILIKI WA DALADALA KUPANDISHA KIWANGO CHA HESABU KWA SIKU KUTOKA SH. 30,000/= HADI 40,000/= WAKATI HAKUNA ABIRIA





Madereva na makonda wamelalamikia pia suala la wamiliki wa Daladala wanazoziendesha kupandisha kiwango cha hesabu kwa Zaidi ya asilimia 30 (30%) wakati huo kukiwa hakuna abiria kitu ambacho kinawafanya wao kumfanyia kazi Boss tu bila wao kuondoka na chochote kwa ajili ya familia zao.





JE MADEREVA WA BODABODA WAO WANAFIDIKA KWA KUPANDISHWA KWA NAULI ZA DALADALA?
Haazu akimuhoji Mkwizu dereva bodaboda


Tumepata pia kuongea na Bw. Mkwizu Adam ambaye yeye ni Dereva wa Bodaboda ambapo naye pia amelalamikia kupandishwa kwa gharama za usafiri kwa daladala na kuweka wazi kuwa wao hawafaidiki chochote kwani abiria wao sio abiria wa daladala bali ni wale abiria ambao labda wana haraka na sehemu wanazokwenda na Alipoulizwa kuwa yeye kwanini anasema kuwa nayeye inamuathiri kwa kumuumiza vipi ambapo yeye alisema kuwa na madereva wa Bodaboda pia wana familia au ndugu ambao wanatumia usafiri wa Dala dala hivyo msumari wake wa mwisho nao akaupigilia palepale kuwa ni bora nauli za daladala zipunguzwe.





BORA NAULI IRUDISHWE ILIVYOKUWA MWANZONI.


Hiyo ndo sentensi ya mwisho kwa kila ambaye amepata kuhojiwa na Waandishi na Watangazaji wa Mambojambo Radio namaanisha Madereva, Makondakta na Wananchi wote wanaiomba Serikali kupunguza Nauli na kurudisha kiwango kilichokuwepo awali pamoja na kuiomba Pia Serikali kuangalia upya mfumo wa Uongozi wa baadhi ya Sekta Zinazosimamiwa na watu Fulani hapa Nchini na mashirika au vyama ambavyo hayaangalia hali ya Mwananchi wa kawaida.
Bw. Deogratius Limo ni Mhariri Mkuu wa MJ FM


Haazu na Mhariri Mkuu wa MJ Radio bw. Deogratius Limo baada ya kutoka mtaani habari zinahaririwa ndo zinakufikia


HAPO CHINI NI BAADHI YA SAUTI ZA WANANCHI, MADEREVA NA MAKONDA TULIOPATA KUONGEA NAO UNAWEZA KUWASIKILIZA.




SHUKRANI KWA UONGOZI NA WAFANYAKAZI WOTE WA MJ RADIO 93.0 FM ARUSHA NA ZOEZI LA WANA MJ KUINGIA MTAANI KUIUNGANISHA SERIKALI NA WANANCHI NI ZOEZI ENDELEZI.

story kutoka HAAZU BLOG.

No comments:

Post a Comment