Friday, April 26, 2013

BUNDUKI 8 RISASI 27 MENO 12 YA TEMBO NA MAGARI MANNE YAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM NDANI YA SIKU TATU

Jeshi la polisi kanda maalum jijini Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 20 ,bunduki  nane na magari manne yaliyoibiwa sehemu mbali mbali ndani ya Tanzania .

Akifafanua mbele ya waandishi 'kamanda wa polisi kanda Maalum Dar es salaam Suleiman Kova, amesema jeshi la polisi kupitia  opereshen iliyohusisha mikoa mitatu ya  Dar es salaam  Yaani Ilala,Kinondoni na Temeke ,kwa ushirikiano na makamanda wao ,wamefanikwa kukamata silaha hizo na watuhumiwa wakubwa 20.

Jeshi la polisi pia limefanikiwa kukamata nyara za serikali zikiwa ni vipande 12 vya meno ya Tembo yenye dhamani ya shilingi milioni thelathin na sita mitano na ishirini katika eneo la kigogo na watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote  mara baada ya  uchunguzi kukamilika .

Aidha kamanda amesema wameweza kukamata zaidi ya risasi 27 katika matukio mbali mbali,moja wapo likiwa ni tukio la kukamatwa kwa watuhumiwa 3 katika eneo la mabibo na mara baada ya kuwapekua waliwakuta na pistol moja ,simu sita ,lain za simu 15 na nguo ambazo hubadilisha baada ya kufanya uhalifu.

Kamanda kova ameendelea kwa kusema kuwa inawashikilia wasichana zaidi ya nane ,mara baada ya kukamatwa wakijihusisha na biashara za kuuza mwili katika eneo la uwanja wa fisi.

Kwa kumalizia kamanda kova amesema jeshi la polisi limeweza kuingizia Taifa zaidi ya millioni 26490 ,mara baada ya kukamata magari 130 kutokana na makosa mbali  mbali ya bara barani na kuwa sisitiza madereva kufuata sheria za barabarani.

No comments:

Post a Comment