Maonyesho ya ndege za kivita yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yakiongozwa na Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali nchini.(PICHA NA IKULU).
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Jakaya Mrisho kikwete amewaongoza watanzania leo kuadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Maadhimisho ya miaka 49 ya muungano yamehudhuriwa na viongozi wa serikali zote mbili ,ikiwa ni marais , viongozi mbali mbali wa kitaifa pamoja na viongozi wastaafu .

Mara baada ya kuwasili kwa mh rais alikagua vikosi mbali mbali vya gwaride la  muungano na kisha mizinga 21 ilipigwa na kufuatiwa na gwaride ambalo lilipita mbele ya rais kwa mwendo pole na mwendo wa kasi. 

Shehe za leo zilipambwa na ndege za mafunzo pamoja na ndege za kivita ,ndege za mafunzo zilipita nakuacha ishara ya moshi wenye rangi za bendera za Tanzania na    kufuatiwa na ndege mbili za  kivita zikipita kwa mwendo wa kasi ikiwa ni ishara  muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Baada ya hapo  ilipita ndege moja kwa staili ya maringo au manuva kwa lugha ya kijeshi na mwisho ilimalizia ndege moja iliyopita kwa heshima na ishara ya utii kwa Rais.

zilifuata burudani mbali mbali kutoka kwa wanafunzi na  vikundi vya ngoma mbali mbali Na kwaya zenye jumbe maalum kuhusu muungano  wa Tanganyika na Zanzibar ambao leo umetimiza  miaka 49.