Friday, August 23, 2013

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI yatoa uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya Polisi, yawavua vyeo baadhi ya Maofisa wa Jeshi hilo kutokana na kukiuka maadili ya kazi zao

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Naibu wake, Pereira Ame Silima.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbaraka Abdulwakili.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Naibu wake, Pereira Ame Silima.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao. Kushoto ni Naibu wake, Pereira Ame Silima. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uchunguzi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wizara yake, ikiwemo kuwafukuza kazi na baadhi yao kuwavua vyeo Askari Polisi waliokiuka maadili ya kazi zao.
 

 
UCHUNGUZI WA MATUKIO YALIYOLALAMIKIWA DHIDI YA ASKARI POLISI KATIKA MIKOA YA ARUSHA, KILIMANJARO, MOROGORO NA KIGOMA

Kati ya tarehe 26 Desemba 2012 na tarehe 18 Mei 2013, yametokea matukio mbalimbali katika Jeshi la Polisi yaliyolalamikiwa na wananchi na kuandikwa kwenye vyombo vya habari. Baadhi ya matukio hayo ni yafuatayo:-

1. Tukio la gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia kutumika katika uhalifu (ubebaji wa bangi) katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

2. Polisi Mkoa wa Morogoro kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kumbambikizia mfanyabiashara kwa lengo la kupata fedha.

3. Mauaji ya mfanyabiashara wa Wilaya ya Kasulu yaliyofanywa na Askari wawili wa Jeshi la Polisi.

Baada ya kuyapokea malalamiko hayo, niliunda Kamati ya kuyachunguza ili kubaini ukweli. Kamati imefanya kazi niliyowatuma na kunikabidhi Taarifa ya Uchunguzi. Baada ya kuipitia Taarifa hiyo kwa makini nimeridhia maoni ya Kamati na hivyo tumefanya maamuzi yafuatayo:

1.0   TUKIO LA BANGI

Tukio hili lilitokea tarehe 18 Mei 2013 majira ya saa tano na nusu za usiku maeneo ya Kilema Pofu katika barabara ya Himo Moshi Mkoani Kilimanjaro.  Kufuastia tukio hilo, waliokuwa Askari Polisi Ex F.1734 Cpl Edward wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha na Ex G.2434 PC George wa Kituo cha Polisi Ngarananyuki, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha walifukuzwa kazi tarehe 20/05/2013 baada ya kukiri kosa la kusafirisha bangi kwa kutumia gari ya Polisi.

1.1 Katika tukio la gari lenye usajili PT 2025 Toyota Land Cruiser la Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha kutumika katika ubebaji wa bangi yenye uzito wa kilogramu 540 zenye thamani ya Tshs 81,000,000/= kukamatwa mkoani Kilimanjaro usiku wa tarehe 18 Mei, 2013, Mkuu wa Kikosi hicho Mkarakibu wa Polisi  Ramadhan Giro amevuliwa madaraka aliyonayo kwa kushindwa kuwasimamia kikamilifu Askari na Maafisa walio chini yake na kusababisha hilo kutokea.

1.2 Kitendo cha Inspekta Isaack Manoni kutuhumiwa kumtorosha mtuhumiwa hatari Ex F.1734 Cpl Edward aliyekuwa dereva wa gari la Jeshi la Polisi lililokamatwa na bangi Mkoani Kilimanjaro ni cha kulifedhehesha Jeshi la Polisi. Hivyo, Inspekta Isaack Manoni amesimamishwa kazi na nimeagiza ashtakiwe kijeshi.

1.3 Kitendo cha Inspekta Salum Juma Kingu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Kilimanjaro kubaki kwenye gari umbali wa mita 80 kutoka nyumba ya mtuhumiwa Ex F.1734 Cpl Edward wakati Cpl Edward alipokuwa amepelekwa kutoka Moshi kukabidhi vifaa vya Jeshi la Polisi, kilichangia mtuhumiwa kutoroka. Inspekta Salum Juma Kingu amepewa onyo na anatakiwa kuwa makini katika utendaji kazi wake.

1.4 Inspekta Mikidadi Galilima hakutimiza wajibu wake ipasavyo katika kumshauri Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha katika ukaguzi na usimamizi wa rasilimali za kikosi. Aidha, kitendo chake cha kujaribu kuficha ukweli kwa kuelekeza matairi mapya yaliyonunuliwa na Ex F.1734 Cpl Edward yavuliwe na yarejeshwe ya zamani kwenye gari PT. 2025 baada ya uhalifu ni cha kukosa uadilifu kama kiongozi. Inspekta Mikidadi Galilima amepewa onyo kali.

1.5 PF 15828 ASP Francis S. Duma aliyekuwa kiongozi katika tukio la kukamata gari ya Jeshi la Polisi lililokuwa limebeba bangi Mkoani Kilimanjaro amepandishwa cheo kuwa Mrakibu wa Polisi kuanzia jana tarehe 21/08/2013.  Aidha, Askari 14 aliokuwa nao siku hiyo ya tukio wapongezwe kwa kupewa zawadi  inayostahili ndani ya mamlaka ya IGP.

2.0    TUKIO LA FUVU

Tarehe 07 Mei, 2013 Askari watatu wa Jeshi la Polisi Ex E.4344 D/Sgt Mohamed na Ex E.3861 Cpl Nuran wa kituo cha Polisi Dumila na Askari Polisi Ex D.4807 D/SSgt Sadick Madodo wa kituo cha Polisi Dakawa wakishirikiana na raia wawili matapeli Rashid Hamis @ Shariff na Adam Peter @ Saloon walimbambikizia fuvu la kichwa cha binadamu mfanyabiashara Bw. Samson Mwita @Kihindi wa Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kupata fedha. Askari hao wamefukuzwa kazi na wameshtakiwa kwa uhalifu waliotenda.

Kabla ya tukio hili Inspekta Jamal Ramadhan ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Mvomero alikuwa na taarifa ya mpango wa kufanyika utapeli katika maeneo ya Dakawa na Dumila ambapo matapeli walikuwa wanapanga kwa kushirikiana na  Askari Polisi wasio waaminifu kuwabambikizia watu kesi kwa lengo la kupata fedha, lakini hakumtaarifu Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila.  Aidha, Mkuu wa Kituo cha Polisi Dumila Inspekta Juma Mpamba ameonesha udhaifu katika utendaji kazi wake kwa kutosimamia kikamilifu Askari walio chini yake, kitendo kilichosababisha Askari hao kujipangia kazi nje ya utaratibu, hivyo kuwa na ujasiri  wa kumbambikizia mfanyabiashara kesi kwa kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kwa lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi. 

Aidha, Inspekta huyu alishindwa kumfuatilia na kumkamata tapeli maarufu Bw. Adam Peter @ Saloon aliyekuwa kinara  wa tukio hili hadi Kamati ilipotoa msisitizo na shinikizo la kukamatwa  kwa tapeli huyo. Kutokana na kasoro zilizoainishwa dhidi ya Inspekta Jamal Ramadhan na Inspketa Juma Mpamba, wote wamevuliwa madaraka walionayo.

3.0  TUKIO LA KASULU

Tarehe 25 Disemba, 2012 usiku wa kuamkia tarehe 26 Disemba, 2012 katika Kituo Kidogo cha Polisi Heru UShingo kilichopo Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Askari Polisi Ex D.8622 Cpl Peter na Ex G.1236 PC Sunday kwa pamoja walimpiga marehemu Gasper Mussa @ Sigwavumba mwenye umri wa miaka 36 na kisha kumweka katika Mahabusu ya Kituo hicho bila msaada wowote wa matibabu hatimaye kufariki tarehe 26 Disemba, 2012 majira ya asubuhi kutokana na kupasuka kwa bandama. Upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho katika kesi ya mauaji dhidi ya Askari hao ambao tayari walikuwa wameshafukuzwa kazi ulisababisha kesi kuondolewa Mahakamani.

Kutokana na kitendo cha Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu ASP Daniel Bendarugaho kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa jalada husika la kesi ya mauaji ya marehemu Gasper Mussa Sigwavumba; ASP Daniel Bendarugaho amevuliwa madaraka aliyonayo.   Aidha, upelelezi wa kesi hiyo utaanza upya ili haki itendeke.

Dkt Emmanuel J. Nchimbi (MB)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
22/08/2013. 

No comments:

Post a Comment