Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia amesema kuwa yeye hapambani wala kukwamisha chama chochote cha siasa bali kusimamia utendaji wa jiji kwa mujibu wa taratibu za nchi.
Mkurugenzi Kihamia amesema kuwa wananchi wa Arusha wasitumie muda mwingi kujadili siasa za majibizano bali wapime kazi kwa vitendo.
Amesema kuwa yeye kama mkurugenzi, mteule wa Rais hatarajii kumwangusha kwa kufanya kazi kwa hofu za vyama vya siasa bali kusimamia uwajibikaji kwa mujibu wa mipaka yake ya kazi.
Kauli hiyo ya Bw Kihamia inakuja kufuatia kile kilichotajwa kuwa ni mvutano wa CCM na CHADEMA baada ya kikao kilichofanyika MEI 25 cha baraza la madiwani wa jiji la Arusha.
Katika kikao hicho mambo mbalimbali ya kimaendeleo yalijadiliwa huku mikakati utatuaji wa matatizo ya wananchi wa jiji la Arusha ikiwemo migogoro ya vibanda 396 vya Stendi Ndogo jiji la Arusha.
Katikamjadala kuhusu mgogoro wa vibanda, Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia aliikataa kamati ya watu wanne iliyokuwa imeundwa na meya wa jiji la Arusha Bw Kalist Lazaro mbele ya baraza hilo la madiwani kwa kile mkurugenzi Kihamia alichodai kuwa madiwani wengi wanatuhumiwa na wananchi kwamba viongozi hao wa kisiasa ndiyo chanzo cha mgogoro.
Kufuatia kwa mkurugezi wa jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia kikataa kamati hiyo iliyokuwa imeundwa na Meya wa jijni la Arusha siku chache baadae M'bunge wa jiji la Arusha Bw Godbles Lema kupitia mtandao wake wa kijamii wa (Instagrame) kupitia account yenye jina la (godbless_j_lema) aliposti maneno yasiyo pungua 56 yenye kusema "Mkurugenzi wa jiji la Arusha jipu anatumika kuuwa upinzani jiji la Arusha.

Maelezo hayo ya Lema yalimtuhumu mkurugenzi kwamba haheshimu maamuzi ya baraza la madiwani kwani anatumika ku influence matakwa ya ccm.
Maelezo hayo yalimkumbusha Mkurugenzi kwamba tunamkumbusha kuwa halmashauri hii niya chadema na matakwa ya chadema ndiyo yanapaswa kusikilizwa, tumeunda kamati mbili za kumshughulikia, halimashauri haiwezi kuongozwa kwa ubabe, magufuli tuondelee huyu mtu kabla hatujamuondoa sisi". (aliposti M'bunge Lema).
Mkurugenzi Kihamia amekumbusha kuwa jamii ikumbukwe kuwa Mkurugenzi Kihamia ni mteule wa Rais wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, na uteuzi wa rais Magufuli ni uteuzi wa weledi na umakini kwa watu wenye uthubutu wa kusimamia ipasavyo serikali.
Amesema kwamba yeye kama mkurugenzi hataruhusu uvujaji wa rasilimali za taifa , bali atasimamia maslahi ya watu bila kujali vyama vyao ama uwezo wao kifedha na umaarufu wao kisiasa.
Arusha hasa eneo la jiji sambamba na utawala wa mkoa kumekuwa na mivutano ya hapa na pale kwani tuhuma za mivutano ya kisiasa na kiutendaji imekuwa ikimuhusisha hata mkuu wa mkoa Bw Mrisho Gambo, mkuu wa wilaya Bw Fabian Daqaro pamoja na mkurugenzi wa jiji Bw Athumani Kihamia huku wao wakisema kuwa wanafanya kazi za maendeleo si siasa za CHADEMA na CCM badala ya UONGOZI UNAOACHA ALAMA.
Mkurugenzi Kihamia amesema mgogoro wa maduka haya 396 yenye migogoro ukiachwa bila ufumbuzi, utapunguza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mapato ya halmashauri ya jiji la Arusha .
No comments:
Post a Comment