Monday, October 10, 2016

MKE WA JACKSON BENT MAREHEMU WINNIE BENT( MAMA JOSHU) KUZIKWA KESHO MAKABURI YA NJIRO ARUSHA




Kufuatia ajali  iliyotokea eneo la Burka nje kidogo ya jiji la Arusha  na kusababisha  mke wa mwimbaji nguli  Jackson Bent kufariki dunia  hatimaye  marehemu Winnie Bent atazikwa kesho jumanne  katika  makaburi ya serikali njiro

Ajali hiyo iliyotokea siku ya jumamosi  ilihusisha basi la Mtei Express na  bodaboda(pikipiki) aliyokuwa amepanda marehemu mke wa Jackson Bent au mama Joshua

Habari kutoka kwa chanzo cha karibu na rafiki wa mume wa mke wa marehemu Mwimbaji Jackson Bent zimeeeleza kuwa  msiba uko nyumbani kwa mwimbaji Jackson Bent Kwa Muorombo

Heshima za mwisho kuuaga mwili wa marehemu Winnie Jackson Benty ama Mrs Benty (mke wa muimbaji nyimbo za injili na kiongozi wa sifa Kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha, Jackson Benty) zitafanyika  kesho Jumanne tarehe 11, maeneo ya Njiro. Msiba ukiwa umewekwa nyumbani kwa marehemu, Kwa Mrombo karibu na bomba la maji ya jeshi.

Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mount Meru, ambapo ibada ya mazishi itaanza saa  tano asubuhi hadi saa saba mchana kisha kufuatiwa na msafara wa kwenda makaburini, Njiro.

Winnie ameacha mgane na watoto wawili, mkubwa akiwa na umri wa miaka mitano.
Jackson na Winnie pamoja na mtoto wao, Joshua

 hakika Mungu ametoa na Mungu ametwaa Jina lake lihimidiwe


No comments:

Post a Comment