Tuesday, October 11, 2016

Rais wa Haiti aelezea madhara ya kimbunga Matthew

Haiti
Rais wa mpito nchini Haiti, Jocelerme Privert amesema kuwa kimbunga Matthew kimeleta uharibifu mkubwa wa miuondombinu na mauaji ya watu wengi.
Amesema kuwa wananchi wa Haiti wanahitaji maji, chakula na dawa haraka sana na mipango ya muda mrefu inahitajika ili kuzuia njaa kuendelea.
Ameongeza kuwa siasa za Haiti zinahitaji kurekebishwa.
Uchaguzi wa Urais nchini humo ulitakiwa kufanyika siku ya jumapili lakini ulishindikana kutokana na kimbunga hicho.
Nchi hiyo imeingia katika matatizo ya kisiasa tangu 2015 kutokana na machafuko na madai ya udanganyifu.

No comments:

Post a Comment