Burundi imewapiga marufuku
wachunguzi watatu wa Umoja wa Mataifa baada yao kuchapisha ripoti
wakiituhumu serikali kwa kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za
kibinadamu.
Wachunguzi hao, kwenye ripoti mwezi jana, walisema
maelfu ya watu waliteswa, wakanyanyaswa kingono au wakatoweka wakati wa
machafuko ya kisiasa yaliyotokea tangu Aprili mwaka jana.Aidha, walitahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mauaji ya halaiki kutokana na kuongezeka kwa machafuko.
Uamuzi huo wa Burundi umetokea siku chache baada ya taifa hilo kutangaza kuwa litajiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
No comments:
Post a Comment