Samsung imetoa wito kwa watu wenye
simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi
kubaini ni kwa nini simu hizo, hata zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa
imethibitisha kwamba ni salama, zinawaka moto.
Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo.Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.
Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama.
No comments:
Post a Comment