Tuesday, April 11, 2017

Korea Kaskazini: Tutatumia ''silaha kali'' kujilinda dhidi ya US



Wanamaji wa Marekani waliotumwa katika eneo la magharibi mwa bahari ya PacificHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanamaji wa Marekani waliotumwa katika eneo la magharibi mwa bahari ya Pacific
Korea Kaskazini imesema kuwa itajitetea kwa kutumia silaha kali ili kujibu hatua ya Marekani kupeleka wanamaji wake katika rasi ya Korea.
Wizara ya maswala ya kigeni ilinukuu shirika la habari la serikali KCNA lililosema kuwa hatua hiyo ya Marekani inaonyesha uvamizi wa kijinga uliofika awamu yenye hatari kubwa.
Jeshi la Marekani katika maeneo ya Pacific limesema kuwa hatua hiyo inalenga kuonyesha Marekani imejiandaa kwa lolote lile.

  • Rais Trump amesema kuwa Marekani imejiandaa kibinafsi kukabiliana na tishio la nyuklia linaloletwa na Korea Kaskazini.
Wakati huohuo Korea Kusini na China ambaye ni mwandani wa Korea Kaskazini wameonya kuchukua hatua kali dhidi ya Pyongyang iwapo itafanya majaribio zaidi ya makombora yake.
Kundi hilo la mashambulizi la Marekani kwa jina Carl Vinson Strike Group linashirikisha meli ya kubeba ndege za kivita.

Lilitarajiwa kuelekea nchini Australia lakini badala yake likapelekwa magharibi mwa bahari ya Pacific ambapo hivi karibuni lilifanya mazoezi ya kijeshi na wanamaji wa Korea Kusini.
''Tutailaumu Marekani kwa matokeo mabaya yaliosababishwa na hatua yake'', ilisema taarifa hiyo ya wizara ya maswala ya kigeni ilionukuliwa na shirika hilo la habari la serikali KNCA.

No comments:

Post a Comment