Mbunge
wa jimbo la Ubungo jijini Dar-es-salaam,John Mnyika,kizungumza kwenye
mkutano wa hadhara uliofayika juzi katika kijiji cha Ndago jimbo la
Iramba magharibi mkoani Singida.Picha na Gasper Andrew
*NI KATIKA MKUTANO WA MNYIKA,MWENYEKITI WA KATA UVCCM AUAWA,18 WAJERUHIWA Raymond
Kaminyoge, Dar na Gasper Andrew, Singida VURUGU kubwa zilizotokea
kwenye mkutano wa hadhara zikiwahusisha wafuasi wa Chadema na CCM
zimesababisha kifo cha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wa Kata ya
Ndago, wilayani Iramba, Yohana Mpinga (30) na majeruhi mmoja.Wafuasi hao
wa Chadema na CCM walishambuliana kwa kutumia silaha za jadi ikiwamo
mawe, wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa unahutubiwa na Mbunge wa
Ubungo, John Mnyika.Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,
Linus Sinzumwa alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kifo cha
mwenyekiti huyo baada ya kupigwa kwa silaha za jadi.Kamanda Sinzumwa
alifafanua kwamba, kutokana na tukio hilo, jeshi hilo linawashikilia
watu 18 wa kata hiyo kwa mahojiano zaidi na watakapobainika kuhusika na
ghasia hizo watafikishwa mahakamani.Alisema majeruhi huyo wa vurugu hizo
anayejulikana kwa jina la Ramadhani Hussein (27), amelazwa katika Kituo
cha Afya cha Ndago baada ya kujeruhiwa vibaya.
“Tukio hilo la
kusikitisha lilitokea Julai 14 mwaka huu saa 10 alasiri katika Kijiji
cha Ndago,” alisema Kamanda.Alisema siku ya tukio, Chadema kilikuwa na
kibali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho na mgeni rasmi
alikuwa Mbunge Mnyika.Kamanda Sinzumwa alisema kuwa, baada ya Chadema
kuanza mkutano huo, viongozi wake walianza kutoa kashfa mbalimbali dhidi
ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwingulu Nchemba.
Alisema
kitendo hicho kiliwaudhi baadhi ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano
huo."Wananchi hao walichukizwa na kitendo cha kukashifiwa mbunge wao na
walianza kupiga kelele kuwa hawataki mbunge wao akashifiwe na badala
yake, wakawataka Chadema wawe wanaeleza sera zao na si vinginevyo,”
alisema.Kamanda huyo alisema licha ya tahadhari hiyo, viongozi hao
waliendelea kueleza kashfa za Mbunge Nchemba na ndipo vurugu zilipoanza.
Alifafanua
kwamba, vurugu hizo zilianza baada ya wafuasi wa CCM waliokasirishwa na
kashfa zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Chadema kuanza kuwarushia
mawe wafuasi wa Chadema. Kamanda Sinzumwa alisema askari polisi wachache
waliokuwapo, walizidiwa nguvu na makundi hayo."Huyu Mwenyekiti wa
Vijana wa CCM, Yohana alikimbilia kwenye nyumba ya Mwalimu Shume Manase
ili kuokoa maisha yake, lakini kundi la wafuasi wa Chadema wakiwa
wamebeba fimbo na mawe, walimpiga sehemu mbalimbali mwilini na
kusababisha kifo chake papo hapo," alisema.
Kamanda huyo alisema
licha ya watuhumiwa 18 kukamatwa, polisi bado inaendelea na msako wa
kuwatafuta watu wengine waliohusika katika tukio hilo ili wafikishwe
mahakamani.Kauli ya MnyikaAkizungumzia vurugu hizo, Mbunge wa Ubungo,
John Mnyika alisema mbinu chafu zinazotumiwa na CCM za kupiga mawe
mikutano yao ya hadhara kamwe haitakidhoofisha chama chao katika
harakati zake za kuwakomboa wananchi kutoka katika maisha magumu.
Mnyika
alisema amefurahi kufika katika jimbo hilo la Mbunge Nchemba kwa sababu
ya propaganda zake, ambazo amekuwa akizitoa bungeni na alivyofanya
ziara kwenye jimbo lake la Ubungo na kuwahutubia watu wa Manzese.Mnyika
alisema wakati wowote kuanzia sasa viongozi wa juu wa chama hicho
watafanya ziara kwenye kata zote za Mkoa wa Singida ili, kuwafahamisha
wananchi hatua za kuchukua katika uchaguzi ujazo.
Nape akataa
kuzungumziaAkizungumzia suala hilo kwa simu, Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema suala la mauaji
lisifanywe kuwa la kisiasa.“Mnataka niseme nini wakati wauaji
wanafahamika? Mtafuteni Kamanda wa polisi awaeleze kuhusu tukio hilo na
hatua zilizochukuliwa, suala hili tusilifanye kuwa la kisiasa,” alisema
Nnauye alipotakiwa kutoa maoni yake.
Mnyika na Nchemba Mvutano wa
wabunge hao lilianza hivi karibuni bungeni baada ya Mnyika kumtuhumu
Nchemba kwamba, ni mmoja wa watuhumiwa wa wizi wa Sh133 bilioni za
Akaunti za Madeni ya Nje (EPA) uliotokea katika Benki Kuu ya Tanzania
(BoT).Kombora hilo la dhidi ya Nchemba ambaye pia ni Mweka Hazina wa
CCM, lilisababisha mabishano bungeni yaliyodumu kwa dakika 20.
Mnyika
alirusha kombora hilo baada ya Nchemba kuchambua bajeti kivuli ya
upinzani kuhusu Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora) na
kukosoa baadhi ya maneno ikiwamo hoja ya kuwa, walimu wanafanya biashara
shuleni kitu akisema kuwa huo ni udhalilishaji wa wanataaluma hao.
Kombora
hilo la Mnyika lilimsimamisha Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama
ambaye alimpa Mnyika siku saba kutoa uthibitisho wa tuhuma alizozitoa
dhidi ya Nchemba.Mnyika alifanya hivyo lakini, Naibu Spika Job Ndugai
alisema kuwa, ushahidi uliotolewa na mbunge huyo hauna mashiko hivyo
kulipeleka suala hilo mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na
Madaraka.E&P
habari na gazeti la mwananchi |
No comments:
Post a Comment