Sunday, June 24, 2012

Polisi wapambana na waandamanaji Sudan

Redio ya taifa nchini Sudan imesema leo kwamba majeshi ya usalama yalitumia hewa ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji kadhaa waliokishambulia kikundi kimoja cha polisi katika mji mkuu Khartoum.

 Ripoti hiyo iliotangazwa leo na Redio Omdurman ilisema kiasi ya waandamanaji 150 walihusika katika kitendo hicho jana usiku na kwamba gari moja la polisi liliharibiwa.


 Awali, upinzani nchini Sudan ulisema  polisi waliyakandamiza maandamano ya kuupinga  utawala wa Rais Omar Hassan al-Bashir, katika  wilaya kadhaa za Khartoum, baada ya sala ya Ijumaa hapo jana.

 Haya yalikuwa maandamano ya siku ya sita ya kupinga mpango wa serikali wa kubana matumizi ambapo bei ya mafuta na chakula imeongezwa maradufu.

 Upinzani unasema mamia ya waandamanaji walikamatwa, katika kipindi cha juma hili, lakini wameachiwa huru.

No comments:

Post a Comment