Wednesday, May 22, 2013

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA YAFANYA SEMINA NA WAFANYABIASHARA WENYE ASILI YA KICHINA

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA ,imeendelea kutoa  semina  juu ya matumizi sahihi ya  mashine za kieletronic za kutoa risit za  TRA,Mashine hizo zilizinduliwa rasmi tarehe 15/05/2013  jiji Dar es salaam katika  hotel ya Serena  ikiwa ni mashine za awamu ya pili kutolewa.

Akionge ana waandishi wa habari  kwenye semina hiyo iliyo husisha  wafanya biashara wenye asili ya kichina ,Afisa  mkufunzi  mwandamizi wa TRA  bwana Hamisi Lupenja ,Amesema semina hiyo   inalenga  kutoa mafunzo  kwa wafanya biashara hao  wa kichina  wanaojihusisha na biashara za uchimbaji wa madini ,ukandarasi wa majumba , upangaji na upangishaji wa majumba.

Semina za TRA zinalenga kuwafundisha wafanyabiashara  kutunza kumbu kumbu zao kwa nji aya kisasa ,ulipaji wa sahihi wa kodi   pia kuhakikisha  wafanyabiashara  wanapata  elimu  ya kutosha  ili kuhakikisha  matumizi  bora ya mashine za kieletronic  ili kuwezesha  serikali  kupata mapato kutokana na biashara zinazofanyika  hapa nchini.

Pamoja na  hayo mamlaka ya mapato TRA , Katika  kuhakikisha  kuwa wanapambana na  changamoto kuhusu matumizi  ya msahine  za kutoa risiti za  kieletronic,Wamejizatiti  katika kutoa semina mbali mbali  ,ambazo zitatoa  fursa  na muongozo  kwa wafanyabiashara  juu  ya matumizi sahihi  ya mashine hizo  za kieletronic  za kutoa risiti za TRA.

Aidha bwana Hamisi amesema wanakutana na changamoto mbali mbali  kuhusu matumizi  ya mashine  hizo  ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara  kusema hawana pesa za kununua mashine hizo  huku wengine wakisema hawajui  kutumia mashine hizo za kieletronic za kutoa risiti za mamlaka ya mapato Tanzania TRA.

No comments:

Post a Comment