Baadhi ya waandishi wa habari, watangazaji na waombolezaji, wakiwa katika msiba huo, nyumbani kwa mama yake mkubwa, marehemu Heny Lyimo leo.
Marehemu Henry Lyimo akiwa katika studio za Moshi fm enzi za uhai wake.
Marehemu Heny Lyimo
Na Paul
Wilium, MOSHI.
WADAU wa
Habari na Michezo mkoani Kilimanjaro, wamegubikwa na siminzi na vilio, baada ya
Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa kituo cha Moshi Fm radio, kufariki dunia.
Mwandishi
huyo, Henry Lyimo alimaarufu Kipesa mchezaji nguli na ghali kuliko wote barani
Afrika, alifariki dunia baada ya usafiri aliokuwa akiutumia wa pikipiki
kugongana na piki piki nyingine katika makutano ya barabara ya Marangu- Rombo,
katika kijiji cha Himo, wilayani Moshi mkoani hapa.
Akizungumzia
kifo hicho, Katibu wa Chama cha waandishi wa Habari (MECKI), mkoani hapa Nakajumo
James, alisema taarifa za kifo cha mwandishi huyo, wa Habari na Mtangazaji,
alizipata Julai 26, mwaka huu majira ya saa mbili za usiku.
James
alisema baada ya kupata taarifa hizo kwa wasamaria wema, alituma mwindishi wa
habari na mtangazaji mwenyake wa kituo hicho, ili kwenda katika eneo la tukio
kuthibitisha taarifa hizo.
Alisema
baada ya mfanyakazi mwenzake kufika katika eneo la tukio alikuta mwili wa
marehemu umeshaondolewa na Jeshi la polisi na kwenda kuhifadhiwa katika
hospitali ya Kilema, ambapo alifwatilia katika hospitali na kukuta taarifa hizo
ni za kweli.
“Baada ya
kupata taarifa za mwandishi mwenzetu wa Habari kufariki dunia, nilipatwa na
mshtuko mkubwa na kuona kama taarifa hizo si za kweli, ambapo nilianza
kuwasiliana na viongozi wenzangu na kuamua kumtuma mmoja wa viongozi kwenda
katika eneo la tukio ili kuhakikisha kuwa taarifa hizo ni za kweli” alisema
Jemsi.
WAANDISHI WA HABARI WALICHUKULIAJE
TUKIO HILI.
Waandishi wa
Habari mkoani Kilimanjaro, wamelipokea tukio hili kwa siminzi kubwa kutokana na
ushirikiano mzuri wa kujitolea wa marehemu huyo ambapo kila mmoja alionyesha
nyuso za siminzi na uzuni mkubwa.
Mmoja wa
waandishi wa Habari na Mtangazaji wa Moshi fm radio, Bahati Mustafa Nyakiraria,
alisema siku ya tukio hilo, majira ya jioni aliwasiliana na Marehemu huyo
akimsihi kuwahi mapema ili waongoze kipindi cha michezo, katika radio hiyo
kinachoanza majira ya saa mbili na nusu za usiku.
“Jana usiku
majira ya jioni, niliwasiliana na Kipesa na kumweleza kuwa tutakuwa nae katika
kipindi cha Michezo majira ya saa mbili na nusu za usiku na kumsihi awahi,
baada ya hapo sikuwasiliana nae paka napokea taarifa za umauti wake” alisema
Mustafa.
Marehemu
huyo ambaye pia alikuwa ni mdau mkubwa sana wa michezo mkoani Kilimanjaro
anategemewa kuzikwa leo (kesho), baada ya ndugu wa marehemu kuwasili nyumbani.
Kamanda wa
Polisi Mkoani hapa, Robert Boaz, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na
kusema kuwa baada ya pikipiki hizo mbili kugongana dereva wa piki piki nyingine
alikimbia kusikojulikana na jeshi la polisi linaendelea na msako ili kumkamata.
Kamanda
Boaz, ametoa pole kwa Familia, Waandishi wote wa Habari mkoani hapa na Taifa pamoja
na wadau wa michezo kwa ujumla kwa kupotelewa kwa mpiganaji nguli kama Henry
Lyimo.
Mungu ametoa
na Mungu ametwaa jina la Bwana lihimidiwe,
kwa niaba ya kampuni ya Jambo Concepts, tunapenda kuwapa pole wafiwa wote na
wadau wa habari na Michezo kote nchini, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki
kizito.
No comments:
Post a Comment