Sunday, August 25, 2013

Taswira za mabango yenye ujumbe wa kila aina uwanja wa taifa Harare, Zimbabwe, siku ya kuapishwa Rais Mugabe


 Asanteni Wazimbabwe kwa kulinda uhuru wa kujiamulia mambo yetu wenyewe
 Zimbabwe kwa Wazimbabwe na Waafrika kwa Waafrika
 Afrika imetamka, heshimuni sauti yake
 Ni nchi ipi ya Afrika iliyosimamia uchaguzi Ulaya ama Marekani?
 SADC, COMESA NA AU wamekuja, wameona na wamethibitisha. Hilo ndilo lenye mantiki kwa Zimbabwe

 Heshimu maoni ya Taifa na Taasisi ya Kitaifa
 Uzawa sasa ni ndoto iliyotimia

 Mtanange sasa ni kati ya Afrika na Ulaya na Zimbabwe ndio uwanja mpya wa mapambano
 Umwagiliaji kwa mikoa yote yenye matatizo ya chakula
 Mungu Mbariki Rais Mugabe kwa msimamo wake usioyumba dhini ya ushoga
 Ni nchi gani ya Africa iliyoendelewa na Magharibi?
 51/49 ndio hesabu pekee tuijuayo (ni kuhusu sera mpya ya uwekezaji ambapo wazawa anakamata asilimia 51 na wageni wanashika asilimia 49)
 Tumepata ardhi sasa tunadai madini yetu
 Ni muda muafaka wa kuunganisha kilichopatikana katika tamko la 1, 2 na 3 la Chimurenga (mapambano ya ukombozi - BOFYA HAPA)
 "Sisi tunaona vizuri zaidi, tunaangalia vizuri zaidi na tunafanya maamuzi vizuri zaidi kuliko nyie wanyeji" (kebehi ya watu wa Magharibi kwa Zimbabwe)
 Nilipiga kura kuchagua uzawa na uwezeshaji
 Zimbabwe haitokuwa koloni tena
 Hongera komredi Mugabe, shujaa wa Afrika

No comments:

Post a Comment