kilele cha miaka hiyo 15 kitaadhimishwa leo na washiriki mbali mbali wa nje na ndani ya nchi ya Tanzania ,wanaojishighulisha na na ujenzi wa majumba,makampuni ya kuuza na kukodisha vifaa na mitambo ya ukandarasi .
Waziri wa ujenzi MH John Pombe Magufuli anatarajiwa kufungua mkutano huo leo asubuhi na kisha kufunga baada ya maonyesho hayo kukamilika ambapo washiriki watapata nafasi ya kuelezea changamoto na mafanikio waliyopata kwa kipindi chote cha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa CRD .
Msajili wa bodi ya wakandarasi bwana Boniphace ametaja baadhi ya changamoto zinazo wakabili kuw ani pamoja na bei ghali katika kulipia kodi wakati wa kununua mitambo ya ukandarasi,uwezo mdogo wa mitaji kwa baadhi ya wakandarasi na makampuni ya ukandarasi,viwango vidogo vya elimu kwa baadhi ya wakandarasi na tatizo la baadhi ya makandarasi wadogo kugushi vyeti ili kuweza kupata kazi kubwa.
akiongea na waandishi wa habari msajili wa bodi ya wakandarasi BONIPHACE MUHEGI amesema leo watajadili kwa makini kuhusu matatizo na mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo ya wakandarasi nchini Tanzania .
Bodi hiyo ya wakandarasi imekumbuka na kutoa pole kwa watanzania wote kwa tukio la kuanguka kwa jengo la ghorofa 15 lililotokea mapema mwaka huu jijini Dar es salaam katika mtaa wa Zananki na Indragandi ,Tukio ambalo liligharimu maisha ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali huku ukiacha watu wengine wakiwa majeruhi.
No comments:
Post a Comment