Polisi nchini Kenya wamekabiliana na waandamanaji waliozingira majengo ya bunge kulaani jaribio la wabunge kutaka kujiongeza mishahara.
Polisi hao wametumia gesi ya kutoa machozi pamoja na maji kuwatawanya waandamanaji hao ambao wengi wao ni wanachama wa mashirika ya kijamii ambao wamesma katu hawaondoki katika majengo hayo ya bunge hadi wabunge watakapopata ujumbe wao.
Maandamano haya yanakuja siku moja baada ya tume ya kitaifa ya mishahara ambayo wajibu wake ni kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa umma kusema kuwa katu haitawaongeza mishahara wabunge.Aidha waandamanaji hao walipeleka Nguruwe kwenye mlango mkuu wa kuingia katika bunge pamoja na damu kama ishara kuwa wabunge ni watu walafi na wasiojali maslahi ya wakenya kwa kujitakia makubwa.
Tume hiyo ilisema siku ya Jumatatu kuwa haitaogopa vitisho vya wabunge kutaka kuivunjilia mbali tume hiyo ikiwa hawatawaongeza mishahara wabunge kama kikwazo.
Wananchi wa Kenya wanaopinga wabunge kuongezwa mishahara
Wabunge hao walijaribu kwa kutumia vitisho kuilazimisha tume hiyo kuwoangeza mishahara lakini hawakufua dafu.
Ni baada ya mbunge mmoja kuwasilisha hoja bungeni kuwa ikiwa tume hiyo haitawaongeza mishahara watafanyya kila hali kuivunja.
Hata hivyo tume hiyo ni ya kikatiba.
Wabunge wa Kenya wanataka kulipwa mshahara wa shilingi 850,000 wakati wakihudumu katika bunge la kumi ikipuuza mshahara waliowekewa na tume ya mishahara ambao ni shilingi 532,000. Wanasema pesa hizi ni kidogo sana.
No comments:
Post a Comment