Monday, January 27, 2014

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA VURUGU ZA GESI NA KUZINDUA MRADI WA MANGAKA

 

na Mwandishi wetu Mercy Edgar
 
MASASI MTWARA
 
Waziri mkuu  mheshimiwa Mizengo Pinda ametembelea maeneo yaliyoathiriwa na vurugu zilizotokea wilayani Masasi tarehe 26.1.2013, na kupelekea uharibifu wa mali zikiwemo nyumba za wabunge, ofisi za halmashauri na jengo la CCM.

Katika ziara yake ya kikazi mkoani mtwara, mheshimiwa pinda ametembelea maeneo yaliyoharibiwa wakati wa vurugu, mwanzoni mwa mwaka jana wilayani masasi na amezindua mradi wa umeme Mangaka, katika wilaya ya nanyumbu,
 
Akizungumza katika ufunguzi wa mradi  huo, waziri mkuu amesema kuwa, dhumuni la serikali ni kila mwananchi wa mjini na kijijini afikiwe na nishati ya umeme.
 
Aidha amesema kuwa mradi wa umeme ni mradi mmoja wapo kati ya miradi sita iliyopewa kipaumbele, ambapo miradi mingine ni kilimo,elimu, maji, uchukuzi na mapato

Katika ufunguzi huo, wazriri mkuu amewapongeza wakandarasi na mamlaka husika zilizofanikisha mradi huo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuilinda miundo mbinu hiyo.

Katika ziara yake mkoani mtwara, waziri mkuu amekagua maendeleo ya ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka mtwara mpaka Dar es salaam na amezindua rasmi mradi wa umeme Mangaka

 

 Waziri mkuu  Mizengo Pinda akiangalia moja  kati ya magari yaliyo chomwa moto nyumbani kwa  Mbuge wa Masasi Mariam Kasembe  wakati wa vurugu mwaka moja uliopita alipotembelea wilaya hiyo.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia Mpira wa Matambara wa kijana Hasani Kasim alipokuwa katika ziara ya kukagua adhari za vurugu mwaka mmoja uliopita katika Wilaya ya Masasi .

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Masasi akimwonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda adhari za vurugu ambapo ofisi ya CCM ilichomwa moto mwaka mmoja uliopita .

 Sehemu ya jengo la CCM Wilaya ya Masasi ambalo liliteketezwa na moto mwaka jana.

 Waziri mkuu  Mizengo Pinda akikagua nyumba ya Mbuge wa Masasi Mariam Kasembe ambayo ilichomwa moto wakati wa vurugu mwaka moja uliopita alipotembelea wilaya hiyo.Kulia ni Omary Lada mume wa Mbuge


Waziri mkuu Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wilaya ya Nanyumbu kulia ni waziri wa nishati na madini Prof Sospeter Muhongo na kutoka kushoto ni Meneja Mwandaminzi wa TANESCO, Kanda ya Dar es salaam na Pwani  inayojumuisha  mikoa ya Lindi na Mtwara Mhandisi  Mahende Mugaya,mkuu wa wilaya ya Nanyumbu, mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal mstaafu Joseph Simbakalia, Mbuge wa Nanyumbu Dastani Mkapa.

No comments:

Post a Comment