Ubalozi wa Marekani nchini Kenya
umeonya kwamba kuna tishio la shambulio la kigaidi kutokea mjini
Mombasa karibuni, na umewataka watumishi wa serikali ya Marekani
kuondoka katika mji huo.
Mwezi wa Oktoba mwaka jana, ubalozi wa Marekani ulisema kuna tishio la shambulio kwenye maeneo ambayo hutembelewa na wageni kama vile maeneo ya maduka mengi na vilabu vya starehe.
Wakati huo hakuna lilotokea, lakini hali katika nchi ya jirani, yaani Somalia, imezidisha wasiwasi.
Marekani imehusika na mapambano dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, ambao baadhi yao wana maingiliano na jamii kubwa ya Wasomali inayoishi Kenya.
Marekani haitaki kupita tena kwenye maafa ya mwaka wa 1998, ambapo ubalozi wake mjini Nairobi ulishambuliwa kwa mabomu, na watu zaidi ya 200 walikufa.
No comments:
Post a Comment