Polisi nchini Pakistan imesema watu wawili waliokuwa na bunduki
wakiwa katika pikipiki walifyatua risasi na kuwauwa watu wanane,
kwenye duka moja la kufuwa nguo kusini magharibi mwa Pakistan.
Afisa wa polisi Salim Shahwani amesema mtu mmoja alijeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea kwenye eneo moja la biashara mjini Quetta, mji mkuu wa mkoa wa Baluchistan.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo, lakini afisa huyo wa polisi amesema waliouwawa walikuwa ni kutoka mkoa wa Punjab.
Mara nyingi mkundi madogo ya wanaopigania kujitenga na mkoa masikini wa Baluchistan yamekuwa yakiwashambulia wakaazi kutoka sehemu nyengine za Pakistan.
Makundi hayo yadai mamlaka zaidi ya kiutawala na sehemu kubwa ya fedha zinazotokana na mali asili za mkoa huo, kama gesi na mafuta.

No comments:
Post a Comment