Monday, June 10, 2013

BONGO MOVIE WAPATA PIGO JINGINE

936957_207421976072897_1906897483_n


WAKATI bado wasanii na  wapenzi wa burudani nchini Tanzania wapo katika majonzi kufutia kifo cha Msanii Albert Mangweha, leo tasnia ya Maigizo na Filamu nchini wamefikwa na janga lingine la kufiwa na Msanii Jaji Khamisi au Kash.

Muigizaji huyo wa filamu na muigizaji Kashi amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Kashi amewahi kutamba na mchezo mbalimbali ya kuigiza katika vituo vya televisheni vya Stars TV akiwa na kundi la Getwell Generation lililokuwa likicheza mchezo wa Hapa ni Bongo na baade kuhamia Kaole na kuonekana ITV akiigiza mchezo wa tamu Chungu na mwisho kuingia  katika uchezaji filamu za bongo maarufu Bongo Movie.

Akizungumza kwa majonzi msanii mwenzake ambaye waliigiza wote katika kundi la Getwell Generation na baadae kuhamia nae Kaole, Halima Yahaya 'Davina' amesema ni kweli Kashi amefariki.

Davina amesema yeye alipta taarifa za kuumwa kwa Kash jana usiku na leo alikuwa akijipanga kwenda kumsalimia Hospitali Muhimbili lakini ghafla akapokea taarifa kuwa Kashi amefariki.

Aidha Davina amesema msiba upo Kinondoni jirani na Bar ya Katumba,  jijini Dar es Salaam ambapo mipango ya mazishi inafanyika.

Akimwelezea marehemu msanii Umy Wenselaus 'Dokii' aliyekuwa kiongozi wa kundi la Getwell na mwalimu wa Maigizo wa kwanza wa msanii huyo amesema kuwa marehemu alikuwa muigizaji mwepesi na aliye na kipaji.

"Ni pigo katika tasnia ya Maigizo maana Marehemu alikuwa na kipaji na mwepesi sana kushika vitu anavyopewa kuvifanyia kazi na hubadilika kulingana na hali ya mchezo,"alisem,a Dokii.

Katika siku za hivi karibuni tasnia ya maigizo imekumbwa na misiba ya kuondokewa na wasanii wake kama Steven Kanumba, Mzee Kipara, Sharo Milionea, Mlopelo na Haji Maganga.

HABARI KWA HISANI YA fatherkidevublog

No comments:

Post a Comment