Sunday, June 16, 2013

DIAMOND AMSEMA MGANGA WAKE KUWA NI MUONGO NA HAMTAMBUI


STAA anayeng’aa katika Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemsuta mganga aliyejitokeza na kudai kwamba mwaka huu staa huyo hatapata mafanikio yoyote na atapotea katika fani. 

Mganga huyo ambaye alidai utaalamu wake ndiyo uliompandisha chati Diamond alisema mwaka huu staa huyo hatapata tuzo, atafifia na jina lake litasahaulika kutokana na kukiuka masharti yake.


Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisisitiza kutomtambua mganga huyo na anamshangaa kwa kuwa mwaka huu amepata mafanikio tofauti na alivyosema.


“Hebu angalieni, mganga alidai mwaka huu nitafutika katika fani, mbona nimepata tuzo mbili kwenye Kil na nimechaguliwa kuwa balozi wa Cocacola na shoo zinajaza kinoma?” alihoji Diamond
.
Aidha, alisema shoo zake bado zinajaza watu wengi huku akiitolea mfano ya mwisho iliyofanyika Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar hivi karibuni iliyojaza nyomi ya watu.



No comments:

Post a Comment