Monday, June 17, 2013

FIFA kuchunguza timu ya Ethiopia


Timu ya taifa ya soka ya Ethiopia
Hali ya ati ati imekumba timu ya taifa ya soka ya Ethiopia huku kukiwa na wasiwasi ikiwa itaweza kuendelea na safari ya kuwania nafasi ya kufuzu kushiriki kombe la dunia nchini Barzil mwaka ujao au la. Hii ni baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kuwachukulia hatua za kinidhani wachezaji wa kikosi hicho Jumapili.
Mapema hapo jana , Ethiopia waliicharaza Afrika Kusini mabao mawili kwa moja mjini Addis Ababa na kujipatia nafasi nzuri katika kinyang'anyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia.
Hata hivyo, kufuzu kwa Ethiopia kunahojiwa baada ya tuhuma kuwa walimshirikisha mchezaji asiyefaa kwenye mechi hiyo ambapo walishinda mabao 2-1wakati walipokuwa wanamenyana na Botswana tarahe nane mwezi Juni. Ikiwa Ethiopia watapatwa na hatia huenda wakapoteza mechi yao waliyocheza dhidi ya Botswana.
FIFA pia inachunguza kikosi cha Togo na kile cha Equatorial Guinea kwa kosa sawa na hilo.
Ikiwa timu hizo zitapatikana na hatia huenda zikaathiriwa vibaya katika kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao Brazil.
Kesi dhidi ya Ethiopia inatia wasiwasi kwani ikiwa watapatikana na hatia huenda ndoto yao ya kushiriki kombe la dunia mwaka ujao ikaambulia patupu huku Afrika Kusini waliokuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010, wakashiriki kwa mara nyingine.
Kwa sasa Ethiopia wako na pointi tano mbele ya Afrika Kusini katika kundi A na Afrika Kusini itakuwa tu na ponti mbili nyuma ikiwa Ethiopia watakubali Bostwana kutwaa ushindi kwa kosa lao la kumchezesha mchezaji asiyefaa au asiyestahili kucheza.
Tangazo hilo la FIFA, halitaipa tu uhai timu ya Afrika Kusini bali wachezaji wa Cameroon na Cape Verde.Cameroon walicharazwa mabao mawili kwa nunge na Togo lakini timu hiyo huenda nayo ikapata pointi tatu zengine ikiwa Togio watapatikana na hatia.

No comments:

Post a Comment