Monday, June 17, 2013

Machel: 'Asanteni kwa kumuombea Mandela'



Hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu

Mkewe rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Graca Machel, amewashukuru maelfu ya watu waliotuma ujumbe wa Ugua pole kwa mzee Mandela
wakati anapoendelea kupoklea matibabu hospitalini.
Alisema kuwa ujumbe huo uliowandolea mzuigo wa wasiwasi na kuleta mapenzi na matumani kwa familia ya Mandela.
Inaarifiwa kuwa Mandela, mwenye umri wa miaka 94, naendelea kupata nafuu ingawa hali yake bado mbaya.
Mandela ambaye ni rais wa kwanza mwusi wa Afrika Kusini amelazwa hospitalini kwa mara ya tatu mwaka huu.
Anasifiwa kwa kuongoza juhudi dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, na kisha kuhubiri watu kusameheana licha ya kuwa alifungwa jela miaka 27. Aliachia madaraka kwa hiari baada ya kuitawala nchi hiyo kwa miaka mitano.
Bi Machel, amekuwa kando ya mumewe tangu alipopalzwa hospitalini, tarehe 8 mwezi Juni kutokana na ogonjwa wa mapafu.
Rais Jacob Zuma alisema kuwa anawaalika watu kumtakia kila la kheri Madiba ingawa bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Bi Machel alisema kuwa dunai imekuwa pamoja naye na kumwezesha kupona.
Tunashukuru sana kwa kila alilofanyiwa.
Mapafu ya Mandela aliyewahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, yaliathirika sana wakati alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya mawe.
Aliugua homa ya mapafu miaka ya themanini wakati akiwa katikia jela ya Robben Island.

No comments:

Post a Comment