Baada ya hapo jana kutokea mlipuko katika viwanja vya soweto kata ya kaloleni jijini Arusha tume ya uchaguzi imeamuru chaguzi ndogo za madiwani kusimama katika kata nne za jiji hilo la Arusha ,kwani wananchi hawawezi kwenda kupiga kura huku wakiwa na hofu ya mlipuko mbali mbali .
akiongea na kituo kimoja cha redio leo asubuhi mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amesema tume imeamua kuahirisha uchaguzi huo ili wananchi waweze kwenda kuwahudumia majeruhi na pia kujipanga upywa kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo ambao leo ungefanyika katika kata 25 .
habari kutoka jijini Arusha zinasema inasiaidikiwa kuwa mlipuko huo ulikuwa na lengo la kuwadhuru viongozi wa chadema lakini kwa kudra za mwenyezi mungu lengo hilo halikutimia na hivyo mlipuko huo kwenda kuwadhuru raia wema wasio na hatia .
jeshi la polisi kupitia kamanda wa polisi liberatus sabas amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo la mlipuko na kusema kuwa hata polisi katika tukio hilo walishindwa kumbainimrushaji wa bomu hilo kutokana na raia kuanza kuwashambulia askari polisi kwa mawe hadi kusababisha magari mawili ya polisi kuvunjwa vioo.
polisi bado hawajadhibitisha idadi ya vifo vilivyotokea kutokana na mlipuko huo unaodhaniwa kuwa ni bomu la kutengenezwa kienyeji na bado msako mkali unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa waliosababisha mlipuko huo jana katika mkutano wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema katika viwanja vya soweto jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment