Tuesday, June 11, 2013

Rais Kikwete awaapisha Mabalozi wawili wapya mjini Dodoma leo


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimuapisha Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo (kulia), kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini China. 
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Balozi mpya wa Tanzania nchini China,  Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo (kulia), mara baada ya kumwapisha, Ikulu ndogo ya Dodoma leo. 
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Balozi mpya wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo (kulia), mara baada ya kumwapisha, Ikulu ndogo ya Dodoma leo. 

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimuapisha Anthony Cheche (kulia), kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Congo DRC, Ikulu ndogo, mjini Dodoma leo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi vitendea kazi Balozi mpya wa Tanzania nchini Congo DRC, Anthony Cheche (kulia), mara baada ya kumwapisha, Ikulu ndogo, mjini Dodoma leo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimpongeza Balozi mpya wa Tanzania nchini Congo DRC, Anthony Cheche (kulia), mara baada ya kumwapisha, Ikulu ndogo, mjini Dodoma leo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu  na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal (wa nne kulia) pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) na Makatibu wakuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo Ikulu ndogo, mjini Dodoma, mara baada ya kuwaapisha Mabalozi wapya wa Tanzania kwa nchi za China na DRC.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakiwa na Mabalozi wapya walioapishwa leo, Juni 11, 2013 katika Ikulu ndogo, mjini Dodoma. Mabalozi hao ni Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo (kulia), anayekuwa balozi wa Tanzania nchini China na Anthony Cheche (kushoto), anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini DRC. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment