Saturday, July 13, 2013

WATOTO WABEBESHWA SILAHA ,CCM WATAKIWA KUJIBU LENGO LA MAFUNZO KWA VIJANA WA GREEN GUARD WAKIWA SILAHA MKONONI

MKURUGENZI WA MAFUNZO WA CHADEMA BW SINGO KIGAILA BENSON AKIONYESHA PICHA YA MWENYEKITI WA CCM AKIKAGUA GWARIDE LILILOANDALIWA NA VIJANA WA ULINZI WA GREEN GUARD WA CHAMA HICHO MKOANI MWANZA HIVI KARIBUNI,JAMBO AMBALO WAMEHOJI KWANINI WAO WANANYIMWA KUFANYA HIVYO HUKU CCM WANARUHUSIWA.
(picha  na exaud mtei wa www.habari24.blospot.com)
HAPA AKIONYESHA WATOTO WA CCM WAKIWA WAMEBEBA KITU AMBACHO AMESEMA NI BUNDUKI NA WAKIFUNDISHWA JINSI YA KUZITUMIA JAMBO AMBALO AMESEMA KUWA NI HATARI SANA KWA AMANI YA TANZANIA(picha  na exaud mtei wa www.habari24.blospot.com)

MAKAO MAKUU YA CHADEMA DAR ES SALAAM(picha  na exaud mtei wa www.habari24.blospot.com)

 Baada ya mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe kutangaza rasmi kuwa chama chake kitatoa mafunzo maalum ya kujilinda kwa vijana wa wao wa ulinzi, na jeshi la polisi kupiga marufuku jambo hilo kwa madai kuwa huo utakuwa ni makosa makubwa,chama hicho kimekuja na jipya baada ya jana mbele ya wanahabari kuonyesha picha ambazo zinaonyesha viongozi wa chama cha ccm wakuwafundisha vijana wao mbinu za kijesha huku wakiwa wamebeba silaha jambo ambalo ni  hatari
 

Akizungumza na waandishi wa habari   mkurugenzi wa mafunzo wa chama hicho amelitaka jeshi la polisi kuanza na ccm badala ya kuwakemea wao kwani vikundi vya ulinzi vya chama vimesajiliwa kwa mujibi wa katiba ya kila chama na ni haki ya mtanzania kujilinda.

      amesema kuwa chama chake hakianzishi vikundi kwani vipo na vimesajiliwa kinachofanyika ni kuwapa mafunzo ya kulinda chama na viongozi wake kwani wamegundua chama chake hakina ulinzi kutoka kwa polisi.
Lakini mkurugenzi huyo alipoulizwa lengo kuu la kuanzisha kikundi hicho na kile kinachosemekani ni kulipiza  mapigo ya ccm ,aliju kuwa wao watatoo mafunzo bila  kutumia silaha.
Wakati maswali yakiendelea ndipo lilipotoka swali kwa mwandishi mwinge je  chama cha demokrasia na mandeleo  kitawapeleka wapi wale wote watakao kamatwa na chama hicho wakiwa katika hatua za kuvunja Amani au kufanya uhalifu  katika mikutano yao .
Jibu kutoka kwa mkurugenzi wa mafunzo bwana Singo ,amesema watapeleka kwa polisi ,
Kwa kweli hali  ni mbaya kwa kila kona , kila mtu anataka ushindi lakini  je hizi roho za watanzania wasio na hatia zinatoketea bila wao kujua kwa katika kile kinachoitwa harakati za ukombozi  nini hatma yake.
Alianza nduguyetu mpenda Mwangosi ,
Akafuata Musa wa Arusha kwa kukatwa na shoka
Bado tukaenda kwenye maadamano wakafa  watatu kwa sila ha za moto  haikuishia hapo  juzi juzi tumepoteza wapendwa wane katika uwanja wa Soweto Arusha  je tunakwend wapi serikali na  viongozi wa vyama vya siasa tuoneeni huruma sisi wananchi tusiojua utamu wa  uongozi wala utamu wa kuishi ikulu kwani tunalea wagonjwa, vijana kwa wazee.

Je unadhani leo likilia boooooooooooooooooooooooooooooom tutakimbilia wapi na ndugu zetu hawa  tafadhali  tuoneeeni huruma watanzania tusio na huruma siasa za chuki na  kuua raia  sio suluhisho la kupata demokrasia  Nchini.

chadema wanauliza  huyu ni kanali wa nchi gani?

je tumefikia kubeba silahi hadi kwenye vyama vya siasa jeshi lipo wapi
 GWARIDE LA KUMALIZA MAFUNZO  VIJANA WAKIWA WAMEKATA  KULIA SHINGO KUTOA HESHIMA KWA MGENI RASMI
vijana wadogo wa green guard ccm

Rais wa jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete  akipokea saluti ya kijeshi kutoka kwa mmoja wa vijana wa green guard CCM.

No comments:

Post a Comment