Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
Na Richard Mwangulube/ Arusha
Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal leo,
amefungua mkutano wa kwanza wa Makazi ulioandaliwa na Jumuiya ya
afrika ya Mashariki (EALA) Mjini Arusha huku akisema suala la makazi
mijini ni changamoto kubwa linalozikabili nchi za bara la Afika.
Makamu wa Rais amewambia wabunge zaidi
ya 150 wanaoshiriki mkutano huo kwamba ili kukabiliana na changamoto
hizo Serikali katika nchi za Bara la Afrika ni lazima ziwekeze
raslimali nyingi katika suala la makazi mijini ili kukabiliana na
chgangamoto ya kuwepo na makazi holela pamoja na mazingira duni.
Dakta Bilal amesisitiza umuhimu kwa
nchi za bara la Afrika kuwa na mipango mizuri ya makazi ili kuwepo na
mipangilio mizuri ya ujenzi, miundo mbinu na amewataka wabunge
wanaoshiriki mkutano huo kuangalia mambo yaliyofanyika katika miaka 25
ya utekelezaji wa malengo ya Melenia (MDGs), kasoro zilizojitokeza
wakati wa utekelezaji wake na miakakti ya kukabiliana nazo.
Aidha, Dakta Bilal amewataka wabunge hao
kuacha kuwa wakosoaji katika Serikali zao tu bali ni lazima wasaidie
kuwa wabunifu katika kuandaa mipango mizuri ya mipango miji.
Amesema suala la makazi mijini ni moja
ya mahitaji muhimnu ya binadamu ambalo linahitaji mtazamo mzuri,
uratibu wa karibu .Hata hivyo amesema hadi sasa katika karne ya 21
bado makazi mengi yamejengwa kwa nyumba za miti, udongo na kuezekwa kwa
majani.
Dakta Bilal amesisitiza kuwa Serikali ya
Tanzania imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za
mipango holela na ujenzi holela, ambapo pia kumekuwepo na kukosekana
kwa huduma zote muhimu za upatikanaji wa majisafi na salama, hudua za
afya na uduni wa mazingira.
Akizungumza katika mkutano huo Rais wa
UN-Habitat Barani Afrika ambaye pia ni Spika wa Bunge la Afrika ya
Mashariki Margaret Nantongo Zziwa amesema mipango duni,kukosekana kwa
maji safi na salama, kukosekana kwa uwekezaji wa kutosha na msongamano
wa makazi ni changamoto kubwa inazikabili nchi za bara la afrika pamoja
na mazingira duni.
Spika Zziwa amesisitiza kwama bara la
Afrika kamwe haliwezi kuw ana ushindani katika dunia kama watu wake
wanaishi kwenye mazingira machafu na makazi duni
Amesema kama Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki ( EAC) ni yetu ni kuhakikisha inaboresha huduma
mbalimbali zinazotolewa kwa watu wetu kwa kuwepo na makazi bora,na
huduma nzuri za afya pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi wa
Tanzania Prof Anna Tibaijuka amesema suala la mazi mijini linahitaji
utashi mkubwa wa kisiasa ili kukabiliana na chanagamoto mbalimbali.
Amesema asilimia 50 ya makazi barani
Afrika haiku katika mpangilio mzuri hali ambayo inatokana na
kukosekana kwa mipango mizuri ya mipango miji.
Amesema katika nchi za afrika hakuna
mipango miji mizuri na kuwataka wananchi kuheshimu sheria hata hivyo
nchi nyingi za afrika hazijawa na mipango miji mizuri ambapo watu
wanadhani ujenzi wa miji ni sawa na ujenzi wa vijijini.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira James Daud Lembeli amesisitiza kuwa masuala ya
ardhi hapa Tanzania ni mali ya Tanzania na sio Jumuiya ya Afria ya
Mashariki.
Mbunge Lembeli amesisitiza kuwa suala
la siasa lisichukue nafasi katika upangaji wa mipango miji katika
nchi za Afrika.Hata hivyo amesema lipo tatizo la baadhi kutoheshimu
sheria za mipango miji, kuvamia maeneo ya wazi na ambayo yanalindwa na
Sheria.
Amesitaka Serikali kuhakikisha sheria za ardhi zinasimamiwa kwa nguvu zote na mamlaka husika bila kuingiliw ana wanasiasa.
No comments:
Post a Comment