Saturday, October 12, 2013

MJUE MKIMBIZA UPEPO CHIPUKIZI MWENYE NDOTO YA KUWA MKIMBIAJI WA KIMATAIFA

 Mkimbiaji chipukizi VICTOR BILAL NTANDU ni mkimbiaji mwenye ndoto ya kufika mbali  mbali katika mchezo wa kukimbizi upepo maarufu kama marathoni
 Victor ni kijana aliezaliwa miaka 27 iliyopita mkoani SINGIDA katika hospital ya MAKYUNGA SINGIDA akiwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto nane wa mzee NTANDU BILAN
 Victor alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Lighwa mwaka 1999 alimalizana kufanikiwa kuchaguliwa klujiunga na shule ya secondary ya Mungaa mwaka 2001 na kumaliza mwaka 2004
 VICTOR alianza kupenda mchezo wa kukimbia au marathon toka akiwa shule ya msingi na hapo alipata nafasi ya kushiriki mashindano ya utashumita  wakati akiwa darasa la tano  katika mashindano ya mbio za mita 5000  na kufanikiwa kushika nafasi y a pili katika mshindano ya wilaya.
  Victor hakuishia hapo alipokuwa secondary aliendelea na upenzi wa mbio za marathon na  mwaka 2003 alishirikia mbio za marathon na kushika nafasi ya 4.

mnano mwaka  2009 alishiriki mbio za kilimanjaro marathon zilizoanzia katika chuo chas ushirika moshi na kupata nafasi ya 19 kwa km 21 mwaka  2012  alishiriki mbio za ROCK CITY za jijini mwanza na kushika nafasi ya 2 katika mbio za km 5.
mpaka sasa VICTOR bado anafanya mazoezi ya kujifua ili kufikia lengo lake la kuwa mkimbiaji wa kimataifa anaomba yeyote yule mwenye nia ya kukuza kipaji chake aweze kumsaidia  kwa vyovyote vile kama kocha au udhamini kamili  kwa sasa victor yupo Dar es salaam akifanya kazi katika kampuni ya ulinzi ya Warrior security  na anaomba yeyote mwenye nia ya kumuendeleza kimichezo aweze kumsaidi
unaweza kumapata kwa namba hizi 0763 188061/0686 0157190

kila la heri Victor mi nakutakia maisha marefu na utimize mal;engo yako ya kupeperusha Bendera ya Taifa  hili Tukufu.

No comments:

Post a Comment