GEOFREY P. SHAID.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George M. Masaju ameshiriki katika hafla ya kiweledi kumuaga Jaji Mstaafu Geofrey P. Shaid. Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar-es-salaam.
Kwenye hotuba yake Masaju amemueleza Jaji Shaid kuwa ni mtu mchapa kazi, kwani mwaka 1973 alianza kazi kama Wakili wa Serikali III hadi kufikia kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Pia aliongeza kuwa jaji Shaid atakumbukwa kwa uadilifu na kutoa maamuzi huru yaliyozingatia weledi.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Jaji Kiongozi Fakihi Jundu wakimkabidhi zawadi Jaji Mstaafu Geofrey Shaidi. Hafla ya kumuaga Jaji Shaid imefanyika viwanja vya mahakama kuu jijini Dar-es-salaam
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju(kulia) akimpongeza Jaji Mstaafu Geofrey Shaid kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar-es-salaam
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju(watatu kulia waliokaa) kwenye picha ya pamoja na Jaji Mstaafu Geofrey Shaid(wapili kushoto waliokaa) |
No comments:
Post a Comment