Sunday, July 20, 2014

Walinzi 20 wa mpakani wauawa Misri


Wanajeshi wa Misri

Maafisa nchini Misri wanasema kuwa takriban walinzi 20 wa mpakani wameuawa katika shambulizi la kizuizi kimoja cha ukaguzi magharibi mwa taifa hilo,karibu na mpaka na Libya.
Duru za usalama zinasema kuwa washambuliaji hao walitumia vifaa vya kurusha magurunedi na silaha kali kutekeleza shambulizi hilo.
Chombo cha habari cha taifa hilo kiliwataja watu hao kuwa watu wanaofanya magendo katika eneo hilo la mpaka huku jeshi likisema kuwa walikuwa wanamgambo.
Maafisa wa usalama wanaamini kwamba wanamgambo kutoka Libya wanajaribu kushirikiana na wapiganaji wa Misri ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi yao katika eneo la Sinai tangu kuondolea madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.

No comments:

Post a Comment