Sunday, July 20, 2014

UN yakabiliwa na ukosefu wa misaada Gaza



Wakimbizi wa Palestina

Umoja wa mataifa umeonya kuwa unakabiliwa na ukosefu wa misaada ili kuwasaidia zaidi ya raia elfu hamsini wa Palestina ambao wameomba hifadhi katika shule za umoja wa mataifa katika eneo la Gaza,ambapo Israel inaendeleza mashambulizi yake ya nchi kavu na angani.
Afisa mmoja anayesimamia oparesheni za misaada ya Umoja wa Mataifa Robert Turner amesema kuwa idadi ya wanaotoroka ni kubwa mno na ilivyotarajiwa na kwamba wakimbizi wapya watalazimika kulala katika sakafu.
Takriban raia mia tatu na hamsini wa Kipalestina wanadaiwa kuuawa tangu Israel ianzishe mashambulizi yake katika eneo la Gaza,ambalo inasema inajibu mashambulizi ya roketi yanayotekelezwa na wapiganaji wa Hamas.
Hapo jana Israel imesema kuwa wanajeshi wake wawili waliuawa baada ya wapiganaji kuingia Israel kupitia handaki moja.

No comments:

Post a Comment