Saturday, December 21, 2013

MABADILIKO YA TABIANCHI YANA MADHARA YA MALI NA UHAI WA BINADAMU - YUNA


DSC_1209
Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), Dr. Lwidiko Edward, akizungumza na vijana kutoka Asasi mbalimbali hapa nchini juu ya ushiriki wa vijana katika mkutano uliopita wa COP 19 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi UNESCO jijini Dar es Salaam.

*Mvua na mafuriko ni mifano hai katika baadhi ya nchi duniani
*Mapigano ya wakulima na wafugaji ni madhara ya mabadiliko ya tabianchi
Na Damas Makangale, MOblog
CHAMA CHA UMOJA WA MATAIFA CHA VIJANA (YUNA) kimesema kwamba mvua, mafuriko na mapigano ya wakulima na wafugaji yanasababishwa na mabadiliko ya tabianchi na kuomba nchi wanachama kuja na mpango mkakati wa muda mrefu kukabiliana na majanga hayo.
Akizungumza na vijana kutoka Asasi mbalimbali za vijana nchini kwenye mkutano wa kujadiliana yaliyojiri katika mkutano wa 19 wa mabadiliko ya tabianchi (COP 19) uliofanyika Warsaw, Poland Afisa Mradi wa Jukwaa la Mabadiliko ya tabianchi, Fazal Issa, amesema kwamba mabadiliko ya tabianchi yamesababisha hasara na vifo kutokana na mvua kubwa zinazosababishwa mabadiliko hayo ya tabianchi.
“kwa mantiki hiyo wanachama kutoka nchi 194 kwenye mkutano wa COP 19 nchini Warsaw, Poland walikubaliana kuja na mkakati wa muda mrefu kushughulikia mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha mvua na mafuriko sehemu nyingi duniani,” amesema.
DSC_1265
DSC_1238
Afisa Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi, Fazal Issa, akiwasilisha ripoti yao ya ushiriki wa vijana na mambo waliokubaliana na wanachama na Asasi za kiraia katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na umuhimu wa kupunguza hewa ukaa duniani.
Issa amesema kwamba moja ya makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi ni kuja na mkakati wa teknolojia na habari ili kuweza kupiga hatua katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia teknolojia zaidi kupunguza hewa ukaa kwenye anga ya duniani.
Amesema pia kwamba katika mkutano huo wajumbe walikubaliana katika kutengeneza mfumo wa kifedha wenye kuwezesha kamati na tume mbalimbali za kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuchangisha fedha kutoka kwa wanachama mbalimbali duniani.
“mpaka sasa kamati ya utendaji wa mabadiliko ya tabianchi imeshakusanya karibu Tsh 33 billioni katika kushughulikia matatizo ya mabadiliko ya tabianchi duniani,” alilisitiza
DSC_1273
Mkuu wa kitengo cha Model UN-YUNA , Adam Anthony, akizugumzia ushiriki wa vijana na Asasi za kiraia katika mkutano wa COP 19 uliofanyika nchini Poland na umuhimu wa wanachama kukubaliana kupunguza hewa ukaa wa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), Dkt. Lwidiko Edward , amesema wamekuja na mkakati wa kutoa taarifa kwa vijana wenzao ya juu ya yaliojiri katika mkutano wa tabianchi na nafasi ya vijana katika kupambana na matatizo ya tabianchi duniani.
Dkt. Edward,  aliongeza kuwa katika mkutano wa COP 19 vijana waliweza kushiriki kikamilifu katika kupeleka agenda zenye maslahi mapana kwa vijana na vizazi vijavyo na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa vijana duniani.
“wanachama wa mabadiliko ya tabianchi duniani wamekubaliana kupunguza hewa ukaa ili kupunguza joto duniani kwa kuanzia ni kwenye nchi zenye viwanda vingi,” amesema.
Amesema pia mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea inaonekana dhahiri kwenye sehemu zenye ukame kwa sasa na mapigano ya wafugaji na wakulima ni mifano hai ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea.
Dkt. Edward, amesema kwamba kupunguza hewa ukaa duniani ni muhimu hata kama baadhi ya nchi tajiri zinategemea viwanda katika kukuza chumi zao na kuleta maendeleo kwa watu wao.
DSC_1250
Vijana wakiuliza maswali mbalimbali juu ya ukweli kwamba Je sauti ya vijana inasikika katika mikutano ya COP duniani.
DSC_1254
DSC_1295
Allyah Mohammed kutoka YUNA, akizungumza kuhusu swala la jinsia na ushiriki wa Mwanamke katika mabadiliko ya Tabianchi kwa sababu wanawake ndio wanaoathirika zaidi na mabadiliko ya Tabianchi duniani.
DSC_1290
Imman Khatib kutoka YUNA akizugumza kuhusu swala la kupata mafunzo mbalimbali kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa vijana na hasa wasichana ili wawe na uelewa kuhusu mambo hayo.
DSC_1278
Sehemu ya vijana walioshiriki mkutano huo ulioandaliwa na YUNA kwa maslahi ya vijana wa Tanzania.
DSC_1227

No comments:

Post a Comment